12 February 2013
Wakulima kuuza korosho kwa bei waitakayo
Na Steven Augustino,Tunduru
WILAYA ya Tunduru Mkoani Ruvuma imebariki ombi la Wakulima wa Korosho la kuuza korosho zao kwa bei yoyote kwa kuiruhusu Kampuni ya Export Treding Ltd iliyokubali kununua korosho hizo kwa bei ya
Sh.1000 kwa kila kilo moja ya zao hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw.Chande Nalicho na kuongeza kuwa maamuzi hayo yametolewa ili kuondoa kero ya wakulima ambao wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu na kwamba baada ya kampuni hiyo kununua korosho hizo zitatakiwa kupelekwa na korosho Africa Ltd zikiwa ni juhudi za Serikali kuhakikisha kuwa kiwanda hicho
kinalipa ushuru na kodi stahiki.
Kwa mujibu wa tamko hilo lililotolewa na DC Nalicho kwa niaba ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo,kampuni hiyo pia imepewa masharti ya kuhakikisha kuwa korosho zote zitakazo nunuliwa
zinabanguliwa katika kiwanda hicho ambapo Serikali itahakikisha kuwa korosho zitakazonunuliwa kwa ulanguzi zinakamatwa na kutaifishwa.
Pia aliwahakikishia wakulima na wananchi wa Wilaya hiyo kuwa atasimamia na kuhakikisha kuwa viongozi
wote wa vyama vilivyofanya vibaya na kusababisha hasara ya bilioni 2.8 zilizotolewa na serikali wanachukuliwa hatua za kisheria.
Alisema kuwa pamoja na kutoa kibali hicho si kwamba Wilaya yake inapingana na msimamo wa serikali wa kutumia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani bali wamefanya hivyo ili kuokoa korosho hizo zisitolewe kwa ulanguzi na kuhakikisha kiwanda hicho kinalipa ushuru katika mfuko wa kuendeleza zao hilo.
Hata hivyo baadhi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tunduru Bw.Hamisi kaesa, Mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya hiyo Bw.Faridu Khamisi na Mwenyekiti wa Mfuko wa Kuendeleza Zao la Korosho Tanzania Bw.Athuman Nkinde walipongeza maamuzi hayo na kuongeza kuwa yatakisaidia kiwanda chao kupata malighafi na kuongeza ajira kwa wananchi wao.
Meneja wa Chamaa Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Wilaya ya Tunduru (Tamco),Bw.Imani Kalembo alisema vipo baadhi ya vyama ambavyo vilisababisha vyama vingine kukosa sifa ya kukopeshekana hivyo katika kipindi hiki watazingatia masuala mbalimbali.
Akizungumzia tukio hilo meneja wa kampuni ya Export Treding Bw.Dinesh Pujaly alisema kuwa katika msimu huu kampuni yake imepanga kununua zaidi ya 6000 kwa ajili ya kuzibangua katika kiwanda chao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment