06 February 2013

Wakazi waishio mabondeni Tegeta waomba viwanja



Na Miriam Sarakikya

BAADHI ya wananchi wanaoishi mabondeni eneo la Tegeta kwa Ndevu, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wameiomba Serikali iwasaidia kuwapa viwanja ili waweze kuondoka katika maeneo hatarishi kutokana na kero wanayopata kipindi cha mvua.


Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti Dar es Salaam juzi, wananchi hao walidai wanashindwa kuondoka maeneo hayo kutokana na ukata wa fedha za kununulia viwanja.

“Baadhi yetu wamejenga nyumba zao katika maeneo haya na wengine wamepanga, tunaiomba Serikali isikilize kilio chetu
ili tuweze kuhamia maeneo salama tofauti na sasa kwani
tunaishi kwa wasiwasi mkubwa,” alisema mkazi wa eneo
hilo Bw. Edgar Msanganzila.

Mkazi mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema hivi sasa eneo lao linafurika maji kutokana na mto uliopo jinani na makazi yao hivyo kuhatarisha maisha yao na familia zao.

Hivi karibuni wananchi hao waliitisha mkutano wa hadhara na kukubaliana kuupanua mto huo maarufu 'Mto Tegeta', ili kupata
njia ya kupitisha maji kirahisi pindi mvua zinaponyesha lakini
hadi sasa mpango huo haujafanikiwa.

No comments:

Post a Comment