11 February 2013

Mwizi wa nazi auawa kwa mnazi



Na Steven William, Muheza

MKAZI wa Kijiji cha Kibanda, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, Ramadhani Abdi, amefariki dunia baada ya kuangukiwa na mnazi
uliokatwa na wananchi wakati akiiba nazi.


Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Constantine Massawe, alisema tukio hilo limetokea mwishoni
mwa wiki kijijini hapo ambapo marehemu alikutwa akiiba
nazi na wananchi waliochoshwa na wizi huo.

“Wakati marehemu akiwa juu ya mnazi, mmiliki wa mnazi ambao nazi zake zilikuwa zikiibwa alifika na kumkuta kijana huyu akiwa
juu hivyo aliita wananchi wakamtaka ateremke lakini alikataa.

“Baada ya kukaidi agizo la kushuka juu ya mnazi kwa muda wa masaa sita, wananchi waliamua kuukata waakati marehemu akiwa
juu hivyo alianguka nao hadi chini na kupoteza maisha,” alisema.

Kamanda Massawe alisema, marehemu alilaliwa na mnazi huo maeneo ya mbavu.

No comments:

Post a Comment