28 February 2013

Muhimbili kushirikiana na NMB kukusanya mapato


Na Rehema Maigala

UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeingia katika makubaliano na benki ya NMB ya ukusanyaji mapato kutoka kwa wagonjwa katika hospitali.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt.Marina Njelekela alisema mchakato huo unaanza kutekelezwa kuanzia Machi 11, mwaka huu.

Alisema kuwa madhumunu ya kuanzishwa kwa utaratibu huo ni kuwepo kwa utoaji wa huduma nzuri kwa wagojwa na kuhakikisha hospitali inakusanya kikamilifu mapato yatokanayo na ada ya mbalimbali zinazolipwa na wagojwa.

"Tumeamua kuingia katika makubaliano hayo ili tupate urahisi wa kukusanya pesa zinazotoka kwa wagojwa na tuweze kutoa huduma bora zinazohitajika kwa Watanzania,"alisema Dkt.Njelekela.

Alisema mabadiliko ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia benki utaongeza makusanyo ya ndani kwa asilimia 50 au zaidi na hivyo kuongeza uwezo wa kifedha kwa kugharamia bajeti ya matumizi ya kawaida kwa kutumia mapato ya ndani kutoka asilimia 58 hadi asilimia 72 kwa mwaka wa fedha 2013-2014.

Dkt.Njelekela alisema makubaliano hayo yalifikiwa baina ya benki ya NMB na uongozi wa hospitali tangu Januari mwaka huu ambapo maandalizi ya kutoa huduma hiyo yalianza.

Naye Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam kutoka benki ya NMB Salie Mlay alisema katika mfumo huu mpya wa kukusanya mapato kutakuwa na vituo vitatu katika hospitali hiyo.

Pia alisema mfumo huo mpya mgojwa atatakiwa kupata hati ya gharama ya malipo ya huduma itakayokuwa inatolewa na wafanyakazi wa hospitali katika vituo vya huduma.

1 comment:

  1. ni mpango mzuri. Ila ndugu wa mgonjwa ndo aende kufanya malipo huko bank NMB wakati mgonjwa anaendelea kupata mataibabu, otherwise mtaua!Edwardo

    ReplyDelete