11 February 2013
Kichanga chatupwa Mabwepande *Chatenganishwa kichwa,kiwiliwili
Na Jesca Kileo
MAITI ya mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya siku 10-15 imekutwa ikiwa imetupwa katika msitu wa mabwepande huku ukiwa umetengana kichwa,mkono wa kulia na kiwiliwili.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Bw.Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea Februari 8 mwaka huu saa 7:00 usiku mwaka huu huko maeneo ya msitu wa mabwepande.
Bw.Kenyela alisema maiti ya mtoto mchanga wa jinsia ya kike ilikutwa ikiwa imetupwa maeneo hayo na mtu asiyefahamika huku mwili huo ukiwa umeharibika kitu kilichopelekea kutengana kichwa,mkono wa kulia na kiwiliwili.
Aidha alisema kuwa maiti imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na hakuna mtu aliyekamatwa,upelelezi unaendelea.
Wakati Omari Seif (32) akiwa anaiba mafuta kwenye tenki la gari aligongwa na gari na kufariki dunia papo hapo.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Bw.Englebert Kihondo alisema tukio hilo lilitokea Februari 8 mwaka huu saa 11:15 asubuhi huko barabara ya Kilwa maeneo ya Kisima cha Serikali karibu na Wipesa Bar Wilaya ya Temeke.
Bw.Kihondo alisema gari yenye no:T 176 AHK aina ya Scania P/Tanker ikiendeshwa na Pius Msigwa(32)mkazi wa Mtongani akitokea barabara ya Kilwa kuelekea Kisima cha Mafuta cha Serikali alimgonga mtembea kwa miguu huyo na kufariki dunia papo hapo.
Alisema kabla ya ajali hiyo marehemu alikuwa amefungua mfuniko wa Tenki la mafuta la gari kwania ya kuiba mafuta,ghafla aliteleza na kuanguka chini hatimaye kukanyagwa na tairi.
Bw.Kihondo alisema maiti imehifadhiwa katika hospitali ya Temeke,dereva amekamatwa na upelelezi unaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment