26 February 2013

Kamanda Mpinga kwa haya bado una kazi



Na Mercy James

IMEELEZWA kuwa ajali za barabarani zimekuwa tatizo kubwa hapa nchini, hasa kutokana na njia za kukabiliana na nazo kushindikana.


Katika kikao cha mwaka cha maofisa wa Jeshi la Polisi kilichoketi kwa siku nne mkoani Dodoma, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Mohammed Mpinga,alikaririwa akisema kuwa ajali hizo zinaisababishia serikali hasara ya sh.bilioni 40 kila mwaka sasa hili ni tatizo.

Kama serikali inakiri kupata hasara hiyo ni wakati sasa wa kutafuta jibu la kudumu juu ya ufumbuzi wa tatizo hilo kwani licha ya serikali kupata hasara pia watu wanapoteza maisha, mali zao na wengine ulemavu wa maisha ambao unazalisha kitu kipya utegemezi na nguvu kazi ya Taifa kupungua.

Barabarani hizi ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara hii ni kutokana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja madereva kutokuwa makini wawapo barabarani ingawa barabara hazi matatizo ya kuwa chanzo cha ajali.

Ajali  hizo ni pamoja na za mabasi yaendayo mikoa mbalimbali ambayo hufanya safari zake kutoka mikoani kuelekea au kutoka jijini Dar es salaamu,na kati zinazotokea zilizo nyingi  zinatokea kwenye  barabara kuu ambazo zina askari wa kikosi cha usalama barabarani.

Kutokana na hali hiyo jeshi la polisi limekuwa likifanya kila kinachowezekana, kubuni mbinu ambazo ziweza kusaidia kuondoa tatizo hilo au kupunguza ajali hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa na visingizio mbalimbali.

Kuna wakati madereva au jeshi hilo hutoa taarifa zisizokuwa na ukweli ndani yake kuhusu  nini chanzo cha ajali kutokea ambapo huwa na visingizio vingi kutoka pande zote mbili.

Katika siku za nyuma kulikuwa na vifaa ambavyo vilikuwa vikijulikana kwa jina la vidhibiti mwendo,(Speed Gavaner) hata hivyo ajali ziliendelea kutokea siku kwa siku na kusababisha vifo vingi visivyovya lazima,na watu kupata vilema vya maisha.

Katika miaka ya 2004/6 mkoani Mbeya kulikuwa na utaratibu wa askari kusindikiza mabasi ya abiria yanayotokea mkoani humo kwenda jijini Dar es Salaamu,ambao walikuwa wakipeana zamu kusindikiza mabasi hayo hai mpakani mwa mkoa huo na Mkoa wa Iringa kwa wakati huo ambao hivi sasa ni Njombe.

Mpango huo ulilenga kudhibi madereva wazembe wawapo barabarani na ulisababisha ajali katika mkoa huo kupungua kwa kiasi fulani kwani madereva wasingeweza kukiuka sheria na kanuni za uendeshaji wakiwa na askari wa usalama ndani ya magari yao.

Hilo lilikuwa wazo hilo lilianzishwa na kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam,Suleiman Kova pamoja na kamanda wa mkoa wa Iringa Advocate Nyombi ambapo mpango huo katika kipindi hicho ulipunguza ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa,ingawa haijulikani ni kwa sababu gani mpango huo usitishwa kimya kimya.

Ni wazi kwamba iwapo askari atakuwa ndani ya basi kuna uwezekano mkubwa kuzuia ajali hizo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nidhamu inafuatwa kwa madereva wawapo kazini.

Moja ya mbinu ambazo zinatumiwa na askari hao sijajua kama ni mawazo ya wakuu au ni mapendekezo ya askari waliopo katika kikosi hicho walitoa ushauri kuwepo kifaa cha kunasa mwendo wa gari likiwa umbali fulani.

Kifaa hicho kinajulikana kwa jina la Tochi kitaalamu (speed raider) kifaa hicho kimepewa majina mengi jina hilo na madereva wa magari,kutokana na uelewa wa wao.

Licha ya kuwepo kifaa hicho haijasaidia kupunguza ajali badala yake zimeongezeka mara dufu watu wengi wanapoteza maisha kupitia ajali zinazotokea na katika mikoa mbalimbali na hivyo kuonekana kuwa hakuna sababu za kuwepo kifaa hicho au kuwepo kwa kifaa hicho si ufumbuzi wa tatizo la ajali hapa nchini.

Nadiriki kusema kifaa hicho kimekuwa mtaji kwa wanaopewa dhamana ya kukishika kwani pale inapotokea uvunjinfu wa sheria mtuhumiwa hachukuli wi hatia za kinidhamu badala yake mtuhumiwa ambaye ni dereva anatakiwa kulipa faini kisha kuendelea na safari.

Ikumbukwe kwamba makosa yanayotumika kunasa kwa kifaa hicho ni mwendo kasi pekee,makosa mengine kama kuzidisha abiria na uchakavu wa gari na mengineyo hayapewi kipaumbele kukaguliwa linatazamwa suala la mwendo kasi pekee.

Naandika uchambuzi huu nikiwa na maana kwamba, kile ninachokisema nakifahamu na nini kinafanyika katika barabara, kuna wakati watu hudiriki kusema, barabara ni mtaji wa askari wa usalama barabarani.

Hii ni kutokana na kile wanachokiona kwa askari barabarani wanapokuwa kazini nini wanafanya, je? tuseme ni uongo yal e yanayosemwa?au tuseme ni fitina za watu kwa jeshi hilo.

Hoja yangu ya msingi kwa wahusika kitengo hicho adhimu Kamanda Mohammed Mpinge, wazo hilo si baya lakini matumizi yake si sahihi, mara nyingi ninaposafiri au ninapokuwa katika njia kuu yaani barabara nakuta vioja pale inapoonekana askari wakimuotea dereva ambaye anaendesha mwendo kwa mwendo kasi na kisha askari hao hujitokeza barabarani ghafla.

Kwa vyovyote vile dereva atakapoona askari mbele yake ghafla atalazimika kufunga breki za ghafla ili kupunguza mwendo sawa na mazingira yanavyoonesha hususani maeneo ambayo kuna alama zinazomtaka aendeshe mwendo gani.

Lakini kutokana na kushtuliwa na askari tochi hulazimkia kupunguza mwendo ghafla ili kukwepa kutozwa faini, ni kweli lengo la kifaa hicho lilikuwa zuri lakini matumizi yake si sahihi.

Nasema si sahihi kwa sababu mbinu zinazotumiwa na askari hao ni mbaya na hatari kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa abiria walio ndani ya gari,ingawa sijajua kimesaidia kwa kiwango gani kupunguza ajali.

Pia kifaa hicho kinaongeza pato lisilo halali hasa pale mharifu anapotozwa fedha kidogo tofauti na kosa ili aweze kuruhusiwa kuendelea na safari, licha kukutwa na makosa, ifahamikwe kuwa dereva anapopoteza muda katika kitua ambacho si rasmi akiruhusiwa huondoka kwa mwendokasi zaidi ya awali kwani anajua kuwa mbele yake hakuna tena kikwazo.

Njia iliyotumika si sahihi kuruhusu askari watumie kifaa hicho kwa kushtukiza, itafutwe njia mbadala ya kumaliza tatizo la ajali lakini njia hiyo badi inahatarisha usalama wa wasafiri.

Kuna wakati nilishuhudia kwa macho yangu madhara ya askari kujificha msituni, au ndani ya gari ili kubaini madereva wanaokwenda kasi waweze kubainishwa na kutokana na kitendo cha askari kujitokeza ghafla barabani kilimfanya dereva ashindwe kusimama ghafla na kusababisha ajali na watu walipoteza maisha katika ajali hiyo.

Sasa basi kwa wale wasiofahamu juu ya kile kinafanyika kwa madereva ni ushirikiano wamekuwa na alama zao wanapopishana, kama kuna askari wa tochi basi wanapashana habari kwa njia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo simu ya mkononi baada ya kubaini kuwepo mahali fulani.
 
Nadhani kuwepo utaratibu wa kufanya ili ajali hizo ziweze kudhibitiwa, mfano kuwazuia wasipokee na hata kupiga simu wawapo barabani hii inaweza kusaidia na njia za kupata taarifa za dereva anayeendesha gari huku akipokea simu ni rahisi zaidi kwa kutumia abiria wenyewe.

Hali hiyo imekithiri miongoni wa madereva hudiriki hata kuandika ujumbe mfupi wakiwa kwenye mwendo jambo ambalo bila shaka ni kosa kisheria, elimu hiyo ni muhimu wananchi wakapewa kama ambavyo kwa mpango wa Polisi jamii ulinzi shirikishi.

Uwepo mpango wa usalama barabarani shirikishi ili kudhibiti hali hiyo, kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaamu  Kova alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi ambao walitakiwa kutoa taarifa iwapo kuna dereva ambaye amekiuka matumizi sahihi ya barabara.

Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa hasa kwa wale ambao walikuwa wakitumia mtindo wa kutanua wanapokuta foleni hutumia njia zisizo halali kufika waendako jambo hilo lilileta shida kwa kipindi lakini ilipotangaza lutoa zawadi kila atakayetoa taarifa za kuwepo kwa dereva aliyeonekana kuvunja sheria na kanuni za usalama barabarani

Ajali hizo zinapotokea si kwamba askari wa usalama barabarani wanakuwa hawapo kazini la hasha wanakuwepo isipokuwa,kuna uzembe unafanyika katika kusimamia suala la kudhibiti mwendo hasa kwa magari ambayo yanasafirisha abiria.

Katika hali hiyo kuna haja gani kuwepo askari kila kituo ambao wanasimamisha magari na kuruhusu yaendelee na safari licha ya kuwepo mapungufu au makosa ambayo yanabainika.

Nashauri kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo hilo ili kuwepo hali ya usalama kama ilivyo kwa nchi za wenzetu japo wa nchi jirani za Malawi, Zambia, Congo na Kenya ambako matukio ya ajali kama kwetu hayatokei mara kwa mara kama ilivyo kwetu.

Nionavyo uwezekano wa kumaliza tatizo la ajali za barabani upo mikononi mwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani, kwa kushirikiana na wananchi ambao wanaweza kuwashiriki wakuu katika kutoa taarifa za uhakika.

Pia kama mbinu ya kusindikiza magari iliweza kupunguza ajali hizo kwanini isiwe mpango endelevu kuwepo askari wa usalama barabarani hata waliovalia kiraia ili kukomesha kabisa tabia ya madereva watovu wa nidhamu ambao hufanya kazi kwa kutumia uzoefu huku wakijua kuwa wanacheza na maisha ya watu na mali zao.

mercyj75@yahoo.com
0789967020


No comments:

Post a Comment