12 February 2013

JK kufungua Mkutano Mkuu wa Polisi




Na Mwandishi Wetu, Dodoma

RAIS Jakaya Kikwete, leo anafungua Mkutano Mkuu wa mwaka
wa Jeshi la Polisi nchini ambao utashirikisha Maofisa Wakuu wa jeshi hilo, makamanda wote wa mikoa na vikosi.


Mkutano huo unafanyika mjini Dodoma na unatarajiwa kumalizika Februari 15 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari mjini humo jana, Msemaji wa jeshi hilo, Bi. Advera Senso, alisema mkutano huo utajadili mambo mbalimbali ya kiutendaji.

Mambo hayo ni pamoja na utekelezaji wa maazimio yaliyoafikiwa katika mkutano wa mwaka 2012 na kuweka mikakati ya namna ya kuendelea kudhibiti, kukabiliana na vitendo vya uhalifu nchini.

Alisema mada mbalimbali zitatolewa na wadau kutoka ndani na
nje ya jeshi hilo ambazo zitalenga kuimarisha uwezo wa namna
ya kuzuia, kupambana na kutanzua uhalifu nchini kuanzia
ngazi ya familia.

“Mkutano huu utahudhuriwa na Mawaziri mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt, Emmanuel Nchimbi,
ukiwa na kauli mbiu inayosema, Tujenge uwezo wa Jamii na
Polisi katika kukabiliana na vurugu kwa kuimarisha utii wa
Sheria bila Shuruti,” alisema Bi. Senso.

No comments:

Post a Comment