11 February 2013
Iran yapongeza uhusiano wake na Tanzania
Na Christina Mokimirya
UBALOZI wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, umedai kufurahishwa na ushirikiano uliopo kati yao na Tanzania
katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Balozi wa Iran nchini, Bw. Mahdi Jafari, aliyasema hayo Dar
es Salaam juzi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya mapinduzi ya nchi hicho.
Alisema nchi hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wake kwa Tanzania ili iweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo sambamba na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta mbalimbali.
“Katika sekta ya biashara, Iran itaongeza mahusiano zaidi ili kutoa fursa kwa nchi hizi kunufaika...mipango ni mingi sana,” alisema.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Rajabu Kahama, alisema ushirikiano uliopo kati
ya nchi hizo ni mzuri kwa maendeleo ya nchi.
“Tumeweza kufungua Kituo cha Afya kilichopo Kigamboni kutokana na uhusiano mzuri wa nchi hizi, kituo hiki kinahudumia waanawake na watoto kwa kutoa matibabu bora,” alisema.
Alisema Serikali ya Iran imeanza mchakato wa kujenga Kituo
cha Ufundi Stadi Zanzibar ambacho kitawasaidia vijana wengi
kuweza kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza mafunzo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment