01 February 2013

ILALA YAANIKA MAFANIKIO YA RAIS KIKWETE

Na Heri Shaaban
WILAYA Ilala imetoa taarifa ya Serikali ya awamu ya nne ya vitu walivyotekeleza kwa kipindi cha miaka saba,ikiwemo  miradi waliosimamia.


Baadhi ya  mafanikio  hayo  kuongeza vituo vya afya,ujenzi wa daraja la Vingugunti,kujenga shule za sekondari 91 kwa kipindi cha miaka saba kuanzia  mwaka 2005 hadi 2013.

Hayo yalisemwa na Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya hiyo Raimond Mushi wakati wa kutoa taarifa ya Serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha miaka hiyo.

Mushi alisema kuwa kati ya shule hizo 91 za sekondari zilizojengwa ambazo zinamilikiwa  na serikali 49 shule zisizo za seriklai 42 kufanya jumla 91.


"Shule za sekondari awali zilikuwa 11 zikaongezwa 80,shule kongwe Pugu, Azania,Tambaza juhudi zilifanyiwa ukarabati ya majengo ya mahabara na vyoo na kuzirudisha katika hadhi yake ya awali."alisema Mushi.


Pia alisema kuwa katika kipindi hicho wamefanikiwa kujenga nyumba za walimu 18 kutoka 52 na kufikia 70 mwaka 2012,Na madawati 9,330 yameongezeka kutoka 14,812 mwaka 2015 na kufikia 24,142  mwaka 2012.

Alisema kuwa katika kipindi hicho pia katika sekta ya afya wamefanikiwa kujenga vituo saba kutoka 15 vya awali na kufikia 22 mwaka 2012 kati ya vituo hivyo vilivyojengwa ni Guluka Kwalala,Bonyokwa,Segerea,Zingiziwa ,Kivule,Gongo lamboto,na Kiwalani.


 Aidha alisema kuwa idadi ya zahanati zimeongezeka kutoka 13 mwaka 2005 na kufikia 20 na na kituo cha afya Mnazi Mmoja kimekarabatiwa,na kupata hadhi ya hospitali ambapo inatoa huduma za mama na mtoto (MHC)na upasuaji pia.

Kwa upande wa hospitali ya wilaya Amana imeongezewa wodi ya wazazi na kuwezesha kulaza wazazi kutoka 30 mwaka 2005 hadi 120 mwaka 2012,ujenzi wa jengo la mapokezi (OPD) ujenzi wa mahabara ya wilaya na jengo la mazoezi kwa wagojwa na mifupa.

No comments:

Post a Comment