01 February 2013

Kaseba aapa kuonesha uwezo wakeNa Mwali Ibrahim

BONDIA Japhet Kaseba, ameapa kuwaonesha Watanzania kilichomfanya bondia, Francis Cheka kumkimbia ulingoni katika pambano lake na Ramadhani Maneno.

Pambano hilo linatarajia kufanyika Machi 2, mwaka huu kuwania ubingwa wa Taifa katika Ukumbi wa DDC Kondoa huku likishuhudiwa na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Japhet Kaseba alisema ameanza kujifua kwa ajili ya pambano hilo, ambapo anataka kuwaonesha Watanzania uwezo wake unaowatisha mabondia wengine na kumfanya wamkimbie, akimtolea mfano Cheka.

"Najua watu wanatamani kuona mpambano huu, ambapo kwa muda mrefu sijapanda ulingoni kutokana na kukosa mabondia wakupigana nao, kwani wamekuwa wakikwepa kupigana na mimi sasa basi pambano hili litadhihirisha hayo," alisema.

Aliongeza kuwa anajifua katika gym yake iliyopo Mwananyamala, ambapo ana imani kwa kuanaza maandalizi mapema kutamsaidia kujiweka vizuri zaidi kwa mpambano huo.

Alisema zaidi anamtaka mpinzani wake ajiandae, ili ushindi huo kwani ana imani atauchukua.

No comments:

Post a Comment