06 February 2013

CHADEMA kuwashtaki Makinda, Ndugai *Dkt. Slaa adai wameshindwa kuliongoza bunge


Na Goodluck Hongo

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, amesema chama hicho
kitatumia ngumu ya umma kupeleka hoja zote za wabunge
zilizokataliwa bungeni kwa wananchi.

Dkt. Slaa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza
na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, hakuna mahakama nyingine za kuwashtaki Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda na Naibu wake, Bw. Job Ndugai.

“Hakuna mahakama yoyote ya wananchi iliyowahi kushindwa, nasi tutapeleka hoja zote zilizozimwa na bungeni na Spika Makina pamoja na Naibu wake Ndugai kwa wananchi,” alisema

Alisema chama hicho kilishatangaza mwaka huu ni wa nguvu
ya umma hivyo kitendo cha Spika na Naibu wake kushindwa kuliongoza Bunge ambalo ndiyo linaisimamia Serikali kwa
kuzima hoja muhimu kwa masilahi ya nchi na Watanzania,
wananchi watatoa hukumu kwa Serikali na CCM.

“Wananchi wanashindwa kupata haki zao mahakamani, polisi na sehemu zingine na hivi sasa vitendo hivi vimehamia bungeni kwa kuzima haki za wananchi.

“Ipo siku uvumilivu utakwisha na kujua kwa nini nchi za Rwanda
na Burundi waliingia vitani...nchi hizi hazijaingia katika vurugu kwa kupenda bali kutokana na ukandamizaji kama huu,” alisema.

Alisema mwaka 2011, aliwahi kusema Tanzania haitatawalika na kuitwa mchochezi lakini leo maamuzi ya Spika ni ya kukandamiza wananchi kwani hoja zilizozimwa ni kwa manufaa ya Watanzania ambapo Spika na Naibu wake, wanaongoza Bunge kwa chuki.

Aliongeza kuwa, kutokana na hilo amewaagiza wabunge wote wa CHADEMA kutokwenda kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hadi Spika atakapoweka wazi rufaa 10 zilizokatwa na wabunge hao.

Aliwataka wajumbe wote ambao watakwenda katika mabaraza ya kutoa maoni ya Katiba Mpya, watoe mani ya kutaka Spika na Naibu wake wasitokane na chama chochote cha siasa ili Bunge liweze kufanya kazi kwa niaba ya wananchi si kwa matakwa ya CCM.

Dkt. Slaa alisema, hivi sasa viongozi wanaoliongoza Bunge hilo, wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa kupindisha kanuni za Bunge wazi wazi na kama zingefuatwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, angejiuzulu.

“Samuel Sitta (Mbunge wa Urambo, mkoani Tbaora na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki), aliongoza Bunge kwa aibu pale alipotaka kupindisha sheria lakini Spika wa sasa na Naibu wake ni balaa zaidi,” alisema Dkt. Slaa.

Alisema cham hicho kinawapongeza wabunge wote wa upinzania waliosimama bungeni kupinga maamuzi ya Spika na hiyo ndio
njia pekee ya kutafuta haki za Watanzania.


1 comment:

  1. MBEGU ALIYOPANDA DR.SLAA [FISADI-[MUASHERATI]]KUVURUGA BUNGE TOKA ENZI ZA SAMWELI SITTA AMBAYE ALIBAKA NAFASI HIYO NI AFADHALI MZEE PIU MSEKWA ANGEENDELEA AMEJENGA UTAMADUNI SIJUI NI BANGI KASUMBA AMBAYO ITACHUKUWA MUDA MREFU KUIONDOA HAINGII AKILINI WABUNGE WA CHAMA KIMOJA MFANO TAWALA KUPINGANA NA MAWAZIRI WAO ULE MSIMAMO WA COLLECTIVE RESPONSIBILTY ULIVURUGWA SANA NA SAMWELI SITTA ,ANNE MAKINDA AMEJITAHIDI SANA KURUDISHA HALI HIYO KAMA NI UONGO MBONA CHADEMA WANATAKA KUWAFUKUZA SHIBUDA NA ZITTO KWA KUKIUKA DHANA YA COLLECTIVE RESPONSIBILLITY KAMA NI UONGO MBONA MWENYEKITI WA BAVICHA TANGA MBONA KAFUKUZWA HII NI DHANA INAYOTUMIKA KATIKA MABUNGE YOTE YALIYO CHINI YA JUMUIYA YA MADOLA SAMWELI SITTA NI MVURUGAJI WA TUTARATIBU HANA ACTION PLAN NI SAWA NA SLAA NI MROPOKAJI MAMBO MENGI ANAYOSEMA NI UONGO[IDEALISM] HAYATEKELEZEKI HANA TOFAUTI NA MAREHEMU PATRICK CHILLUBA WA ZAMBIA ALIPEWA URAIS NA KUONDOLEWA HARAKA SI VIZURI KUFANYA MAJARIBIO YA KUFA

    ReplyDelete