07 February 2013

Airtel yatangaza walioshinda Mamilionea


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mawasiliano Airtel jana, imetangaza washindi wa promosheni ya Amka Millionea na kuwazawadia wateja wake mamilioni ya pesa taslimu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema promosheni inaendelea na kuwataka wateja wao wanatakiwa kushiriki.

Alisema jinsi ya kushiriki mteja anatakiwa kutuma neno shinda milionea kwenda namba 15595.

"Kuna zaidi ya sh. milioni 150 zimebaki kwa ajili ya wateja kujishindia, hadi itakapofika mwisho wa promosheni hii," alisema Mmbando.

Aliwataja baadhi ya washindi walioshinda promosheni hiyo ambao wanatoka Dar es Salaam kuwa Emmanuel Mndeme, Salima Hassan, Jamali Kahema na Veronica Mrema.

Wengine walioibuka washindi kutoka mikoani ni Novatus Majura kutoka wa Kagera, AbdulAbbas Joshua, Frederick Shirima, Joseph Bombo na Sapuro Mollel wa Arusha.

"Hii ni maalumu kwaajili ya wateja wote wa Airtel nchi nzima, hivyo tunawashauri wale wote ambao ni wateja wa Airtel, au wanatamani kuijiunga nasi wahamie sasa ili wafurahie kuamka mamilionea," alisema.


No comments:

Post a Comment