11 February 2013
Ahukumiwa miaka 16 jela kwa ubakaji
Na Raphael Okello, Musoma
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi, mkoani Mara, imemuhukumu Bw. Amiri Bakari (18), kifungo cha miaka 16 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri wa
miaka 16 (jina tunalihifadhi).
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bi. Janeth Msaroche, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa polisi, Jonas Kaijage kuwa, Bw. Bakari alitenda kosa hilo Januari 10,2012 katika eneo la
Vailet Bar, iliyopo Mtaa wa Nyakato, mjini Musoma.
Bw. Kaijage aliieleza mahakama hiyo kuwa, kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ni kosa la jinai hivyo aliiomba itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Kutokana na ombi hilo, Hakimu Msaroche alitoa adhabu ya mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 16 gerezani. Kesi hiyo
ilifikishwa mahakamani hapo Februari 7,2012.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment