Na Lilian Justice,Morogoro
WANANCHI Mkoani Morogoro wametakiwa kutumia kikamilifu mvua zinazoendelea kunyesha kwa kulima mazao yanayostahili ukame na yale yanayokomaa muda
mfupi ili kuepukana na baa la njaa.
Hayo yalisemwa jana mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa wa Chama cha Wakulima Kanda ya Mashariki (TASO) Bw.Mohamed Mzee wakati akizungumza na gazeti hili
mjini hapa.
Mzee alisema kuwa wananchi mkoani hapa wanatakiwa kuzitumia vyema mvua zinazoendelea kunyesha katika kupanda mazao mbalimbali ikiwemo yale yanayokomaa kwa kipindi kifupi badala ya kubaki na kasumba ya
kulima mazao yanayokomaa muda mrefu.
"TASO inapenda kuwahimiza wananchi kuzitumia vyema mvua hizi kwani wakishindwa kufanya hivyo watashindwa kuzalisha mazao yanayokidhi mahitaji
yao, "alisema Bw.Mzee.
Pia aliwaasa wananchi kuepuka kuuza mazao ya ghalani kiholela kwani wataweza kujikuta wakikabiliwa na baa la njaa kutokana na tabia ya
mabadiliko tabia ya nchi .
"Ni vyema wananchi wakatambua kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanaweza kutokea na endapo watakuwa ameuza mazao yote ya ghalani watashindwa kuvuna
mazao ya kutosha, "alisema Bw.Mzee.
Kwa upande wake katibu wa TASO Bw.Rafaeli Jackson aliwataka wenye mabanda au vipando ndani ya Uwanja wa Maonesho ya Kilimo wa Julius Kambarage Nyerere kuhakikisha wanasafisha mabanda na pia kuotesha mboga mboga ili kuweza kuzuia wananchi kuharibu maeneo.
"Nawahimiza wenye mabanda na vipando kutunza na kulima mboga mboga kwenye vipando vyake badala ya kusubiri Maonyesho ya Nanenane,"alisema.
Hata hivyo alisema kuwa TASO inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wanachama kushindwa kulipa ada zao sambamba na kushindwa kuendeleza mabanda
ndani ya uwanja wa maonesho ya kilimo .
No comments:
Post a Comment