31 January 2013

Vijana FC yapenya nusu fainali



Na Omary Mngindo, Kibaha

VIJANA FC ya Kongowe Kibaha mkoani Pwani, juzi imeingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mikoba Cup,
inayoendelea katika Kata ya Misugusugu wilayani hapa.

Timu hiyo inayoundwa na vijana wenye umri chini ya miaka 17, imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya
Magita FC.

Washindi hao walijipatia bao hilo la pekee dakika ya 86 kupitia kwa Digi Kazi, aliyeunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Judi Ally.

Kwenye michuano hiyo mshindi wa kwanza, atajipatia jezi na wa pili ataondoka na mbuzi.

Michuano hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuibua na kuviendeleza vipaji, ndani ya kata mbalimbali zilizomo wilayani hapa.

Akizungumzia mafanikio hayo, Mlezi wa Vijana FC, Juma Nduya alisema
amefurahishwa na maendeleo ya timu yake, hivyo amewaomba wadau kujitokeza kuwasaidia vifaa vya michezo kwa ajili ya kuwandeleza vijana hao.

“Nitumie nafasi hii kuwaomba wadau mbalimbali, kujitokeza kuisaidia timu
hii kwani imekuwa na mafanikio lukuki, lakini inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vifaa kama jezi, bukta, viatu na vingine vingi,” alisema Nduya.

Alisema klabu hiyo, iko tayari kuvaa jezi za mfanyabiashara yeyote atakayejitokeza kuwadhamini, ili wamtangazie biashara zake.


No comments:

Post a Comment