03 January 2013
'Tumieni dini zenu kuombea amani'
Na Damiano Mkumbo
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone, amewataka wakazi wa Mkoa huo kutumia imani ya dini zao kuombea
amani na utulivu nchini.
Dkt. Kone alitoa wito huo jana katika mkesha wa kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 uliofanyika kwenye Viwanja
vya Namfua, ambao uliandaliwa na umoja wa makanisa ambao
unafahamika kwa jina la Tanzania Fellowship Churches.
“Nawaomba mzingatie mafundisho yote yaliyopo katika vitabu vya dini pamoja na kutii sheria za nchi, mlinzi wa kwanza wa amani ni mwananchi mwenyewe,” alisema.
Katika mkesha huo, Wachungaji na Maaskofu walifanya ibada maalumu ya kuombea Taifa kuwa na amani ambayo ndio msingi
wa maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Naye Askofu Paul Samweli, alisema mwaka 2013 haugawanyiki kihesabu hivyo hakutakuwa na kitu chochote kitakachowagawa Watanzania kidini, kisiasa wala kikabila.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment