21 January 2013


Na Zahoro Mlanzi

WAREMBO 40 wanaowania taji la Miss Utalii 2013 kutoka mikoa mbalimbali nchini, wameripoti kambini tayari kwa kambi ya siku 21 kwenye hoteli ya Ikondelelo Lodge, Kibamba Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa shindano hilo, alisema warembo hao wakiwa kambini watapata mafunzo na semina mbalimbali kuhusu utalii, utamaduni, uwekezaji, afya ya jamii, elimu ya jamii na ulinzi shiriki.

"Warembo hao watakuwa chini ya jopo la wakufunzi la mashindano haya wakiongozwa na Mkufunzi Mkuu, Erasato Gideon, pamoja na Mkufunzi Mkuu wa Ngoma za Asili, Mariam Kweji kutoka Kundi la Sanaa la Kaole, Mkufunzi wa Muziki na Dansi, Asuku Che Mundugwao, Wakufunzi wa minato na miondoko ya urembo na mitindo, Caroline Mrosso na Evamary Gamba," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Alisema kambi hiyo itaanza rasmi leo na kuwataja baadhi ya warembo waliongia kambini na mikoa wanayotoka ni Rose Godwin wa Arusha, Sophia Yusuph Dar es Salaam 1, Ivon Stephen Dar es Salaam 2, Irine Thomas Dar es Salaam 3, Erica Ekibariki Dodoma, Hamisa Jabiri  Geita, Debora Jacob Iringa, Elline Bwire Kagera 1, Jania Abdul Kagera2, Mulky Uda Kagera 3 na  Anna Poaly wa Kilimanjaro.

Wengine ni Joan John wa Lindi, Halima Hamis wa Mtwara, Dorine Bukoni wa Mara, Mary Lita wa Manyara, Diana Joachim wa Mbeya, Jesca Peter wa Mwanza,Hadija Said wa Morogoro, Sarafina Jackson na Leah Makange wa Tanga,Magreth Malalle wa Tabora, Pauline Mgeni wa Njombe, Anganile Rogers wa Rukwa na Asha Ramadhani wa Katavi.

No comments:

Post a Comment