03 January 2013
Mkakati wa uzazi wa mpango uwe sambamba na matumizi rasilimali
Na Darlin Said
MKAKATI wa uzazi wa mpango uliotolwea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete kwa lengo kupunguza ongezeko la watu ili Serikali isiwe na mzigo mkubwa wa kuhudumia uende sambamba na matumizi bora ya rasilimali.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mbunge wa jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjaro Bw.Agustino Mrema alipokuwa anazungumza na gazeti hili kuhusiana na matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012 ambapo watanzania wanakadiriwa kuwa zaidi ya mil.44 .
Bw.Mrema alisema ingawa idadi ya Watanzania imeongezeka kwa kiwango kikubwa bado rasilimali zilizokuwepo zinajitosheleza kuwahudumia wananchi hata kama wataongezeka zaidi ya hapo.
Alisema wakati umefika kwa Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaohusika na matumizi mabaya ya pesa za umma na rasilimali ili kila Mtanzania anufaike na mapato ya Serikali.
Alisema ni lazima kupambana na wezi na mafisadi ili kuepusha mipango hewa kwani wanaiba huku akitolea mfano kutengenezwa barabara nje ya viwango.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment