03 January 2013
Mil. 55/- kujenga soko la kisasa Tandale
Na Rehema Maigala
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, imetenga sh. milioni 55 kwa ajili ya ujenzi wa sko la kisasa
la Tandale.
Mwenyekiti wa Chama cha Wauza Nafaka Ndani na Nje ya Nchi (TAMAGRASAI), Bw. Juma Dikwe, aliyasema hayo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika mdahalo wa kupeana mbinu za kufanya biashara ulioshirikisha Maofisa Biashara, Kamati za Masoko na wafanyabiashara mbalimbali wa jiji hilo.
Alisema halmashauri imetenga pesa hiyo ili kulifanya soko hilo ambalo ni la muda mrefu liwe na hadhi tofauti na ilivyo sasa.
“Soko la kisasa litatusaidia kupata wateja kutoka sehemu mbalimbali kwani tutakuwa tukifanya biashara na watu tofauti wa ndani na nje ya nchi,” alisema Bw. Dikwe.
Diwani wa Kata ya Tandale, Bw. Jumanne Mbunju, alisema tayari halmashauri hiyo imekamilisha michoro ya soko hilo pamoja na kutangaza tena kwa ajili ya ujenzi huo.
Hata hivyo, Bw. Mbunju alisema kujengwa kwa soko hilo kutaongeza mapato ya halmashauri hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment