17 December 2012

Watupwa jela miaka 30 kwa kunajisi, kulawiti



Luppy Kung’al,Polisi na Raphael Okello,Musoma.


WATU wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na makosa ya kunajisi na kulawiti watoto wawili wenye umri wa miaka 12 katika matukio mawili tofauti yaliyotendeka Mikoa ya Dodoma na Mara.


Katika tukio la kwanza Mahakama ya Wilaya Kongwa, mkoani Dodoma ilimhukumu, Jumanne Hassan (22) kifungo cha miaka 30 na kuchapwa viboko 30 kwa kupatikana na kosa la kunajisi mtoto wa darasa la tano.

Aluehukumiwa adhabu hiyo ni mkazi wa Kijiji cha Liganga, Kata ya Chitego tarafa ya Nzoisa. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya kongwa, Godfrey Pius, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa.

Awali ilidaiwa na Mwandesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi, Maulid Manu, aliieleza mahakama jinsi mtoto huyo alivyonajisiwa huku akitishiwa kuuawa iwapo atapiga kelele.

Alidai kuwa kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 1, mwaka jana saa mbili na nusu usiku katika Kijiji cha Liganga, Kata ya
Chitego na Tarafa ya Nzoisa Wilayani Kongwa.

Wakati huo huo, Mahakama ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, imemhukumu kifungo cha miaka 30, Adam Godfrey (27) kwa kosa la kumlawiti binti wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyambono Wilaya ya Musoma Vijijini.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mfawidhi Mwandamizi Wilaya ya Musoma, Richard Maganga, alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuridhika na utetezi wa upande wa mashtaka, hivyo anamhukumu Adam Godfrey, kutumia kifungo hicho.

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali, Jonas Kaijage, aliieleza  mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo katika Kijiji cha Sagana Musoma vijijini Mei 11, mwaka huu ambapo alimuingilia mbinti huyo kinyume na maumbile.

Kaijage alisema Godfrey alikuwa akinywa pombe ya kienyeji kwa mama wa binti huyo, hivyo baada ya kunywa alidai hakuwa na hela hivyo aliomba ampe mtoto wake aende naye nyumbani kwake ili ampatie fedha anazodaiwa.

Alidai wakiwa njia, Godfrey alimtishia kisu binti huyo kisha kumlawiti. Kesi hiyo ilifikishwa na kusomwa kwa mara ya kwanza  mahakamani hapo Juni 12, mwaka huu.


No comments:

Post a Comment