21 December 2012
Wanaondekeza makundi CCM kukiona-Kalogeres
Na Lilian Justice,Morogoro.
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Morogoro,Inocent Kalogeres ameahidi kula sahani moja na mwanachama yeyote atakaebainika kuwa ni kinara wa kuendeleza makundi ndani ya chama hicho.
Kauli hiyo aliitoa mjini Ifakara katika uwanja wa Kiungani kwenye mkutano wa hadhara kuutambulisha uongozi mpya wa chama hicho mkoa na kujiimarisha kisiasa ziara inayofanyika katika wilaya zote mkoani humo.
Alisema kinachoichafua CCM hivi sasa ni makundi yanayoendelezwa na wanachama wenye uchu wa madaraka ambayo ikiwa yataachiwa yatakihatarisha chama hicho katika chaguzi zijazo ukiwemo wa serikali za mitaa 2014 na kuchaguzi mkuu 2015.
Mwenyekiti huyo aliwaagiza viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya matawi kuwasaka mamluki wote na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwawajibisha ili kuondoa misuguano kabla ya kufika kipindi cha chaguzi hizo.
Kuhusu baadhi ya viongozi wa vijiji kutosoma taarifa za mapato na matumizi,Kalogeres aliwataka wahusika kufuata taratibu za kusoma taarifa hizo na atakaeshindwa atafute pori la kwenda kwa kuwa uvumilivu ndani ya chama umekwisha.
Akizungumzia zoezi la uondoaji mifugo na wakulima katika bonde la Kilombero alisema halina nia mbaya isipokuwa kulinusuru bonde hilo na kulifanya kuendelevu na kutunza bio anuai ambapo pia aliitaka Serikali kuwatafutia eneo mbadala watu wote waliokuwa eneo hilo.
Aidha alitoa miezi sita kwa Halmashauri za wilaya mkoani humo kuondoa kero ya maji katika miji ukiwemo wa Ifakara sambamba na miezi tisa kuboresha huduma za hospitali kuondoa adha aya afya kwa wanachi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,Hassan Masala alitaja miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa kama ilani ya chama hicho na kukanusha upotoshaji unaofanyika juu ya operesheni ya okoa bonde la Kilombero.
''Mpaka sasa ni mifugo laki 3 imeondolewa toka zoezi hilo lianze na linazingatia sheria na kusema kuwa wapo viongozi wanaoendesha kampeni za kupotosha wananchi wasiondoe mifugo na kusema kuwa wao hawatawaachia viongozi hao''alisema Masala..
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa hata kama mifugo inayoendelea kukamatwa hivi sasa ikibainika kuwa ya kiongozi wao hawatasita kuikamata na kuipiga faini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment