21 December 2012
Pinda aahidi kuchangia mil. 25/- za jenereta
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda, ameahidi kuchangia gharama za ununuzi wa jenereta katika Kata ya Majimoto, Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi ili wakazi wake wapate umeme wa uhakika.
Bw. Pinda alitoa ahadi hiyo juzi wakati kata hiyo akiwa katika
ziara yake ya siku saba jimboni kwake Katavi.
“Kuna wafanyabiashara hapa Majimoto ambao walikuja kuniona na kusema wapo tayari kuchangia ununuzi wa jenereta lenye uwezo wa kutoa kilovoti 60 za umeme kwa nyumba kama 300.
“Kama watakuwa tayari kutoa sh. milioni 25 na mimi nitachangia kama hizo, kaeni na kupanga namna ya kuchangia gharama baada
ya muda fulani mtakuta mmemaliza kuchangia, tuwarudishie wafanyabiashara hela yao ili hilo jenereta liwe la kijiji.
Mkilipata nitawasiliana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ili watupatie nguzo za umeme,” alisema.
Akijibu hoja ya viwanja, Bw. Pinda ambaye ni mbunge wa Jimbo la Katavi, alisema upimaji wa viwanja ulifanyika miaka miwili iliyopita na kupatikana 270 lakini havijagawiwa kwa wananchi na kuwataka viongozi wa kata na Wilaya wasimamie kazi hiyo.
Bw. Pinda alitumia fursa hiyo kuwaonya juu ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara kando ya barabara kuu. “Ninawaomba sana muheshimu sheria za barabara...msijenge nyumba zenu ndani ya hifadhi ya barabara,”
Jana Bw. Pinda aliendelea na ziara yake katika Kata ya Usevya ambako atazindua mradi wa umeme jua (solar power), kwenye Sekondari ya Kata ya Usevya na kuhutubia wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment