MAMLAKA ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu(SUMATRA) imefichua siri za kuzama kwa meli nchini kuanzia ile ya Mv. Bukoba na zingine ambazo zimeendelea kutokea katika Bahari ya Hindi na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.
Akizungumza wakati wa semina ya wadau wa majini na wamiliki wa meli nchini, Mkuu wa kuratibu huduma za utafutaji na uokoaji SUMATRA Kapteni Ken Chimweji, alisema ajali nyingi zinazotokea majini zinasababishwa na uzembe wa kibinadamu.
Alisema kwa kawaida inatakiwa kabla ya meli kuanza safari kukaguliwa ili kuepusha madhara wakati wa safari.
Alisema vifo vingi vinavyotokea kwenye ajali hizo vinasababishwa na binadamu wenyewe, kwani kabla ya kuanza safari ikaguliwe ubora wake, ikiwa ni pamoja na kujua imebeba abiria wangapi na ina uwezo wa gani wa kubeba wasafiri na mizigo.
Ukiangalia kuanzia ajali iliyopotokea Mei 21, mwaka 1996 meli ya Mv.Bukoba iliyokuwa inatokea bukoba na kwenda Mwanza ilikuwa haijafata kanuni za na sheria za meli jinsi zinavyotaka.
Meli ile ilibeba mizigo mingi tofauti na uwezo wake wa kubeba mizigo iliyokuwa imebeba na pia ilikuwa imebeba abiria wengi vilevile meli ile ilikuwa na ubovu hivyo isingemudu kubeba mizigo iliyobeba ni lazima ingezama tu.
Lakini hiyo yote imetokana na meli hiyo kung'oa nanga bila ya kuchunguzwa kitu chochote kile ili kumfikisha abiria akiwa salama yeye na mali zake alizobeba katika meli hiyo"alisema Chimweji
Kwa upande meli Inspice Islander iliyokuwa inatoka Dar es salaam kwenda Pemba chanzo cha ajali ilikuwa ni abiria kuwa wengi katika meli hiyo kuliko uwezo wa meli yenyewe.
Tume ya iliyochunguza meli hiyo ilisema kuwa meli hiyo ni chakavu ilitengenezwa mwaka 1967 mwaka 2007 Tanzania walinunua meli hiyo ambayo tayari ilikuwa chakavu na ilikuwa haina uwezo wa kubeba abiria wengi.
Lakini Tume hiyo ilisema kuwa meli hiyo ilibeba zaidi ya abiria 2000 ijapokuwa nahodha wa meli alisema uwongo kuwa meli ilibeba watu 500.
MELI YA Mv.Skagit sababu za kuzama kwa meli hiyo ilikuwa ni hali ya hewa katika bahari siku ya tukio kulikuwa na upepo mkali hivyo meli ya aina hii isingeweza kuhimili mawimbi makali ndio sababu za kuzama kwa meli hiyo.
Meli hii ilikuwa inauwezo wa kuchukua abiria 250 tu,na jinsi ilivyo ilikuwa haina uwezo wa kwenda safari za mbali kama yenyewe ilivyofanya,siku ya ilivyopata ajali meli hiyo ilibeba abiria zaidi ya 400.
Hata hivyo Kepteni Chimweji alisema hali hiyo pia inasabaishwa na wafanyakazi wa melini kutopewa mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuendesha vyombo hivyo usalama.
Alisema kuwa mikataba ya kazi nayo inachangia kutokea kwa ajali za mara kwa mara baharini.
Utamkuta nahodha anafanya kazi hana mkataba wowote na kampuni yake hali hiyo nayo inasababisha nahodha huyo asifanye kazi kwa ufanisi .
Watu wengi hupoteza maisha pale meli inapozama kwa sababu ya nohodha kutotoa taarifa haraka sehemu zinazohusika.
Hivyo inatakiwa Wizara zinazohusika kuweka kanuni na sheria kali ili kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara kwa sababu ya uzembe.
Naye, Hussein Mohamed Saidi Meneja Mkuu wa meli za Azam alisema kuwa,miundo mbinu ni mibovu hivyo inakuwa ngumu hata kumuweka mwekezaji kwa ajili ya kuleta meli yake ili aje kuifanya kazi Tanzania.
"Mpaka hivi sasa hakuna hata sej Kampuni ya meli
No comments:
Post a Comment