20 December 2012
Serikali yaifungia Hotel ya Double Tree *Yadaiwa kutiririsha maji taka baharini
Na Waandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Terezya Huvisa, jana ameifungia Hotel ya Double Tree ya Dar
es Salaam kutokana na kutiririsha maji taka baharini.
Dkt. Huvisa alitoa agizo la kuifungia hoteli hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Charles Kitwanga.
Ziara hiyo ililenga kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa
awali juu ya hoteli hiyo kuweka mfumo wa maji taka.
Katika ziara hiyo, Hotel ya Double Tree iliagizwa kuwa na mpango wa muda mfupi na haraka wa kusitisha utiririshaji wa maji taka baharini ambao hadi jana ilikuwa haijatekeleza agizo hilo.
Sambamba na hilo, Dkt. Huvisa pia amefuta ukaguzi wa Mazingira na kuitaka hoteli hiyo kurekebisha mara moja mfumo huo pamoja na kulipa faini kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment