20 December 2012

Ofisa Afya afungiwa kwenye ghala

Patrick Mabula,Kahama,

OFISA afya wa Wilaya ya Kahama Bw.Charles Mwaipopo , juzi alijikuta katika wakati mgumu baada ya kufungiwa kwenye ghala la kuhifadhia bidhaa kwa zaidi ya masaa matano alipokuwa akifanya ugaguzi.


Bw.Mwaipopo alifungiwa kwenye ghala la mfanyabiashara Bw. Lucas Kishimbe ambae alikiri kumfungia ofisa afya huyo alipokuwa amekwenda kukagua bidhaa zilizopo katika ghala hilo .


Mfanyabishara Bw. Kishimbe alisema aliamua kumfungia ofisa huyo baada ya kutishia kuziteketeza bidhaa zilizomo humo kama asingetoa chochote  kwa madai hazina ubora  toka viwandani ambako huzinunua.


Bw.Kishimbe alisema ofisa huyo alifika katika ghala lake  na kujitambulisha kuwa anakuja kufanya ukaguzi  na alimfungulia hadi ndani lakini akihumo aliomba apewe pesa  ndipo alipogoma na kumtishia kuziteketeza bidhaa zilizomo humo.


Alisema baada ya kupewa vitisho hivyo ndipo alipoamua kumfungia ndani ya ghala lake na kuomba msaada kwa mkubwa wake Ofisa afya wa wilaya Bw .Athanas Ng’oboko  ambae alimkana kumtuma kufakazi hiyo  na kutoa vitisho ili apewe chochote.

Ofisa afya wa wilaya Bw.Ng’oboko alipoulizwa alikiri kufungiwa ndani kwa  ofisa huyo na kumkana kuwa siyo mfanyakazi katika Halmashauri ya wilaya bali ni wa Halmashauri ya mji  na kuwa hakutuma kwenda kufanya kazi hiyo ambayo alisema huenda alikuwa alikuwa na mpango wa kujipatia pesa toka kwa mfanyabishara huyo aliyefungia kwenye ghala.


Naye Ofisa afya wa Halmashauri ya mji wa Kahama Bw.Marten Masele alipoulizwa naye alikiri kuwepo kwa tukio hilo lakini alimkana Bw.Mwaipopo kuwa hayupo chini ya halmashauri hiyo na wala hajamtuma kwenda kufanya ukaguzi kwenye maghala ya bidhaa za wafanyabishara mjini kahama.


Kwa upande wake Afisa huyo  Mwaipopo alikiri kufungiwa ndani ya ghala la Bw.Kishimbe na kueleza  kuwa yeye alikwenda  hapo kufaatia maagizo ya Mamlaka ya Chakula na Dawa “TFDA’”kutoka jijini Mwanza kwamba Mfanyabiashara huyo  anatabia ya kuingiza bidhaa zisizokuwa na kiwango cha ubora ,hali ambayo aligoma kukaguliwa.

Bw.Mwaipopo alisema akiwa amefungiwa kwenye gahala alipiga simu kwa maofisa wenzake ambao walifika hapo wakiwa na askari polisi ndipo  walipomwokoa na alipofunguliwa na mfanyabishara huyo .

Hata hivyo habari za kuaminika na za siku nyigi toka kwa baadhi ya wananchi na maofisa afya katika Halmashauri za wilaya ya Kahama na ya mji wa Kahama  , asilimia kubwa wafanyabishara wilayani hapa  wamekuwa na mchezo mchafu kwa kwa siku nyingi huwa wanachakachua bidhaa  katika madhala yao hali ambayo inahatarisha afya za watumiaji.

No comments:

Post a Comment