20 December 2012
Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi azidi kusota
Na Eliasa Ally, Iringa
MTUHUMIWA wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi ambaye aliuawa
katika kijiji cha Nyololo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo alifikishwa mahakamani hapo akiwa katika gari la mahabusu wengine tofauti na siku zilizotangulia hali ambayo imeleta mshangao kwa watu waliohudhuria kusikiliza kesi hiyo.
Mtuhumiwa huyo Pasificus Cleophace Simon (23) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma ya kumuua kwa makusudi mwandishi huyo wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa uliofanyika May 2 mwaka huu.
Akisomewa mashtaka na Mwendesha mashtaka wa serikali Adolf Maganda aliiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Dyness Lyimo kuwa upelelezi wa mauaji ya Daud Mwagosi bado haujakamilika na kesi imeahilishwa hadi 03 Januari, 2013 itakapotajwa tena.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo Desemba 6 mwaka huu mtuhumiwa huyo Pasificus Cleophace Simon hakufikishwa mahakamani kwa kudaiwa kuwa gari ambalo lilitakiwa limlete lilikosa mafutautokana na sababu iliyotolewa kuwa gari la kusafirishia mahabusu limekosa mafuta.
Baadhi ya wananchi wakizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo walisema kuwa vitendo vinavyofanywa na maaskari katika kumlinda zaidi mtuhumiwa huyo kwa kumleta kwa gari la peke yake badala ya kutumia karandinga la kuchukua watumiwa kuwa vinamfanya mtuhumiwa huyo kuonekana kesi yake ipo tofauti na wauaji wengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment