21 December 2012
NHC latangaza kuuza nyumba zake Kibada
Na Goodluck Hongo
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limetangaza rasmi kuanza kuuza nyuba zake zilizopo eneo la Kibada, Kigamboni na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa shirika hilo Bw. David Shambwe, alisema muda wa kununua nyumba hizo ni kuanzia
Januri 2,2013 ambayo ndio siku ya wananchi kuanza kuzilipia.
Alisema nyumba zitakazoanza kuuzwa ni 182 ambazo kati ya hizo zipo zenye vyumba viwili na vitatu ambapo mradi huo umegharimu zaidi ya sh. bilioni 6.6 hadi kukamilika Mei 2013.
“Nyumba zenye vyumba viwili zina ukubwa wa mita za mraba
56, katika eneo la mradi pia kutakuwa na maduka, shule za awali, viwanja vya mazoezi, yule anyehitaji kununua aende katika ofisi
zetu za shirika zilizopo karibu naye,” alisema Bw. Shambwe.
Alisema wanunuzi wa nyumba za vyumba viwili wanapaswa
kulipia sh. milioni 3 za awali kabla ya kupewa barua ya ofa
ambapo gharama halisi ya nyumba hizo sh. milioni 39.8 na
nyumba za vyumba vitatu zinauzwa sh. milioni 45.5.
Aliongeza kuwa, katika eneo la mradi kuna nyumba 290 na ujenzi huo ulianza Novemba mosi mwaka huu 2012 ambapo Rais Jakaya Kikwete alifika eneo la mradi na kuzizindua.
“Wote ambao watapata nafasi ya kununua nyumba hizi, hawaruhusiwi kuzibomoa wala kubadilisha mfumo wake
kwani zimejengwa kwa kuzingatia sheria mpya ambayo
Rais tayari ameisaini,” alisema Bw. Shambwe.
Alisema nyumba zinazouzwa ni zile za bei nafuu na wale ambao watazilipia watapewa barua ambazo zitawawezesha kupata mkopo
benki ili waweze kumalizia fedha zilizobaki ambapo muda wa
ziada ni miezi mitatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment