21 December 2012
Makandarasi 2,008 wafutiwa leseni zao
Na Mariam Mziwanda
ZAIDI ya wakandarasi 2,008 wamefutiwa leseni zao na kufungiwa kufanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kutokana na utendaji mbovu wa kazi na kutotimiza matakwa ya mikataba
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma ambao utagharimu sh. bilioni 3 ambazo ni mchango wa Serikali kwa kutambua umuhimu wa
makazi bora kwa wananchi.
“Mahitaji ya nyumba bora nchini yanakadiliwa zaidi milioni 3
nchi nzima na ongezeko la mahitaji ni nyumba 20,000 kila mwaka, watumishi wa Serikali pekee ni zaidi ya 400,000 hivyo juhudi za Serikali na sekta binafsi zitasaidia kuziba mwanya huu,” alisema.
Aliwataka watumishi wa umma ambao wamepata kipaumbele cha kupangishwa nyumba na wakala wa majengo nchini, wazitumie vizuri ili kupunguza gharama za ukarabati ambazo zinaweza kutumika katika shughuli nyingine.
“Wale waliokopeshwa na kuuziwa nyumba, mzilipe kwa wakati ili kumjengea uwezo wakala wa kujenga nyumba nyingine kwa manufaa ya umma,” alisema.
Akizungumza katika ghafla hiyo, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, alisema kutokana na sheria namba 17 ya mwaka 1997
ya wakandarasi, Serikali haitasita kuendelea kufuta leseni za wakandarasi wabovu ili kulinda heshima ya kazi hiyo.
Alisema Serikali itaendelea kuwapa tenda wakandarasi wa ndani ili kukuza uchumi wa nchi na kuongeza fursa ya ajira kwa wazawa na kumtaka mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kuhakikisha anaendelea kujenga kwa viwango na kumaliza ujenzi kwa wakati.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini, Elius Mwakilinga, alisema malengo yaliyopo ni kuhakikisha kila mwananchi anaishi katika mazingira bora hivyo mwaka huu watajenga nyumba 2500
ambapo Dar es Salaam mahitaji ni nyumba 1,400.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment