13 December 2012
Nabaki Africa yapongezwa kutoa mafunzo ya ufundi
Na Jamaal Mlewa
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Bw. Raymond Mushi, amefurahishwa na hatua ya uongozi wa kampuni ya kusambaza
vifaa vya ujenzi ya Nabaki Africa Limited, kutoa mafunzo ya
ufundi kwa wafanyakazi wake.
Bw. Mushi aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua tawi jipya la kampuni hiyo lililopo Kariakoo.
Alisema kampuni hiyo huagiza vifaa halisi vya ujenzi kutoka nchi
za Italia, Dubai, Afrika Kusini, Argentina, Milki za Kiarabu (UAE), New Zealand na Malaysia.
Aliongeza kuwa, hatua ya kumpuni hiyo kutoa mafunzo kwa wafnyakazi wake juu utumiaji wa vifaa vinavyoagizwa kutoka
nje ni jambo la kuigwa na kampuni nyingine zilizopo nchini.
“Hii inatuongezea idadi ya watalaamu wa kutumia vifaa hivi, pengine tungelazimika kutuma watu nje ili kwenda kujifunza matumizi na matengenezo ya vifaa husika,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Hamish Hamilton, ameipongeza Serikali kwa
juhudi zake za kupiga vita uingizwaji bidhaa bandia nchini.
Aliwataka wateja hasa wa bidhaa za ujenzi kuwa makini wanaponunua vifaa kutoka nje ambavyo vingi ni bandia.
“Sisi ndio wakala pekee wa bidhaa ambazo zinatengenezwa na Kampuni ya Decra kutoka New Zealand, ukizunguka kwenye maduka utaona bidhaa hizi zimejaa,” alisema.
Meneja Uwendeshaji wa kampuni hiyo, Bw. Joseph Massae, amesema tatizo la uingizwaji bidhaa bandia nchini linafanywa
na wafanyabiashara waaminifu na changamoto iliyopo ipo katika
bei za bidhaa husika.
Alisema hivi sasa kampuni hiyo ina mkakati wa kufungua matawi sehemu nyingi nchini ili kukidhi mahitaji ya wateja kwa urahisi.
Kampuni hiyo ina matawi Mbezi Beach, Masaki na Kariakoo jijini Dar es Salaam. Matawi mengine yapo katika miji ya Mwanza, Arusha, Moshi, Tanga na Mtwara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment