24 December 2012
Mgimwa ahamasisha ujenzi wa bweni
Na Eliasa Ally, Iringa
WAZIRI wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, amewataka watendaji jimboni humo pamoja na diwani wa Kata ya Luhota, kuhamasisha wananchi ili waweze kujenga bweni la wanafunzi wa kike.
Bweni hilo litasaidia kuwaepusha wanafunzi hao kupata mimba kabla ya kumaliza masomo yao kama ilivyo sasa.
Dkt. Mgimwa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Kata ya Luhota, wakati akizungumza na wananchi na kuchangia mabati 100, pamoja na mifuko 50 ya saruji.
Alisema kama wanafunzi wa kike watajengewa mabweni na kuhudumiwa chini ya walimu, wataweza kutimiza ndoto za
kuhitimu kuhitimu na kufaulu vizuri masomo yao.
Dkt. Mgimwa alisema vitu hivyo vina thamani ya sh. milioni
3.6, na kuwataka watendaji, diwani pamoja na wananchi kuona umuhimu wa kuchangia katika sekta ya elimu.
Aliongeza kuwa, wanafunzi wengi wanaosoma sekondari hiyo, wanaishi kwenye nyumba za kupanga ambapo hali hiyo inawafanya wanafunzi wa kike kupata vishawishi pamoja na ujauzito.
“Kama watajengewa mabweni, wanafunzi wa kikekuwa chini ya uangalizi wa walimu wao na kuwawekea utaratibu maalumu kama zilivyo sekondari zingine za bweni, wengi watatimiza ndoyo zao na kufikia malengo ya kujielimisha,” alisema Dkt. Mgimwa.
Aliutaka uongozi wa Serikali Kata ya Luhota, kuwasimamia wananchi ili kuanza mara moja kuchimba msingi wa bweni la wanafunzi wa kike 300 ili waanze kuyatumia na baadaye
watajenga mabweni ya wavulana.
Aliongeza kuwa, kuhusu maabara ya sekondari hiyo ataiboresha ili iwe ya kisasa kuliko ilivyo sasa kwani wanafunzi wanatumia vifaa duni kufanya majaribio katika masomo ya sayansi hivyo itakuwa vigumu kufikia malengo yao kutokana na uduni wa vifaa husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment