24 December 2012

Mfumo wa maji taka bado ni tatizo-Kitwanga



Na Rachel Balama

USAFI wa mazingira ni njia ya kuendeleza afya kwa njia ya kuzuia mawasiliano ya binadamu na athari za taka.Athari zinaweza kuwa za kimwili, mikrobiyolojia, biyolojia au kemikali

Taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na wanyama, taka ngumu, maji machafu, taka za viwandani na taka za kilimo.

Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote.Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa athari za afya ya wote katika kaya na katika jamii.

Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratibu ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa taka na maji machafu.

Tatizo la mifumo ya maji taka kwenye viwanda na hoteli katika Jiji la Dar es salaam limekuwa ni tatizo na hiyo inatokana na miradi hiyo kuanza kabla ya sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 .

Zamani maeneo ya viwanda yalikuwa yakitengwa maalum ambapo  yalikuwa na mifumo mizuri ya maji taka tofauti na sasa ambapo viwanda vingi vipo kwenye makazi ya watu.

Viwanda kujengwa kwenye makazi ya watu inatokana na maeneo mengi ya mijini kutokuwa na nafasi za kutosha jambo linalopelekea athari kwa  binadamu na viumbe vingine.

Kwa kuwa viwanda vina mahitaji makubwa ya kuzalisha hivyo ni lazima na hali ya uchafu itaongezeka, kutokana na kuongezeka huko basi inahitajika miundombinu thabiti ya kuhakikisha kuwa maji taka hayatililishwi kwenye makazi ya watu.

Katika kuhakikisha suala la usafi linashughulikiwa hapa nchini Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Charles Kitwanga pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Udhibiti wa Mazingira,walifanya ziara ya ghafla kwenye viwanda na hoteli zilizopo pembezoni wa bahari ya Hindi Jijini Dar es alaam ambapo alijionea hali halisi ya mazingira hasa kwa upande wa mifumo ya maji taka.

Watu wanawajibu wa kulinda nchi na kupata maendeleo lakini ni lazima shughuli hizo zisiharibu mazingira na kusababisha maafa kwa upande mwingine.

Kwa upande wa viwanda, hali ni mbaya kwa kuwa Waziri  Kitwanga alijionea  changamoto nyingi kubwa ikiwa ni baadhi ya viwanda kukosa mashine za kusafishia maji taka kwa kiwango kinachotakiwa na kisha kuhurusiwa kutiririshwa kwenye mito,bahari na mireji.

Kitwanga, amesema  wanaotililisha maji taka kwenye mito, mifereji na  baharini bila kufuata taratibu za sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004  watakuchuliwa hatua.

Anasema kuwa maendeleo  yasisababishe binadamu kupotea,Hata hivyo Kitwanga ameto maagizo kwa NEMC kuhakikisha wanakaa na viongozi wa viwamda na hoteli ambazo zimeonekana kuwa na mazingira yasiyo salama kuhakikisha wanarekebisha.

Anasema changamoto mbalimbali alizokutana nazo zimesababishwa na sheria ya mazingira kuchelewa kwa kuwa viwanda vingi vilijengwa kabla ya sheria hiyo.

Anasema maeneo yaliyotengwa kwa viwanda yalikuwa na mfumo wa maji taka ambapo asilimia nane viliunganishwa lakini kwa sasa haupo.

Anasema miundombinu ya maji taka imezidiwa kutokana na kukosekana kwa kukithiri kwa viwanda.

Katika ziara hiyo Kitwanga, alitembelea kiwanda cha TAN PACK, MMI Steel, BIDCO, Cocacola Kwanza, Shelly's Pharmactical, ambapo amejionea baadhi ya viwanda hivyo kutokuwa na mitambo ya kusafisha maji taka pamoja na teknolojia ya kuondoa rangi kwenye maji taka.

Katika kiwanda cha dawa cha Shelly's Pharmactical, aliagiza Baraza la Usimamizi na Udhibiti wa Mazingira (NEMC) kukaa pamoja na viongozi wa kiwanda hicho na kurekebisha karoro zilizojitokeza.

"Kaeni na uongozi wa kiwanda na mkubaliane kuondoa kasoro ndogo ndogo," anasema.

Aidha pia ameagiza kiwanda hicho kufanyiwa ukaguzi wa mazingira ili kujua ni hatua zipi zichukuliwe kwa lengo la kujikinga na madhara.

Hata hivyo  Kitwanga alivutiwa na kiwanda cha Soda cha Cocacola Kwanza kutokana na kuwa na mitambo maalum ya kusafishia maji kwa kiwango kinachotakiwa ili kuruhusiwa kutililishwa kwenye mitaro.

Pia ameuomba uongozi wa kiwanda hicho kutoa mafunzo kuhusu usafi wa mazingira kwenye viwanda vingine kutokana na kiwnda hicho

Kwa upande wa hoteli ametembelea hoteli ya Giraff,, Double Tree,  Coral Beach, Africana, Sea Cliff na nyinginezo.

Amekutana na changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni baadhi ya hoteli kutiririsha kinyesi baharini  ambapo moja ya hoteli hizo ni Double Tree ambapo aliagiza hoteli hiyo kurekebisha mfumo wa maji taka mara moja.

Mbali na kuagiza mfumo huo urekebishwe pia Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche, aliutaka uongozi wa hoteli hiyo kubomoa makaro ya maji ya kinyesi yanayoingia baharini pamoja na kulipa faini isiyopungua milioni 50.

Pia Kitwanga ameagiza kusimamisha ujenzi wa hoteli inayojengwa karibu  Giraff hadi watakapofanya ukaguzi wa mazingira kutokana na hoteli hiyo kuweka viroba vya mchanga kwenye ufukwe wa bahari na kusababisha taka kujikusanya sehemu moja na kutozolewa kwa muda mrefu.

Ametoa onyo kwa wenye hoteli ambao wamekuwa wakiwazuia wafanyakazi wa  NEMC kutofanya kazi ya ukaguzi kwenye hoteli zao kuacha.

"NEMC leteni taarifa za hoteli zote zinazowazuia ninyi kuingia  kwa ajili ya ukaguzi wa mazingira, ole wao," aliagiza.

Hata hivyo Kitwanga, amekiri kuwa mfumo wa maji taka katika viwanda na hoteli Jijini Dar es salaam kuwa ni tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa

No comments:

Post a Comment