24 December 2012

Mathew 'TBS Original': *Msanii wa Hip Hop aliyechungulia kaburi *Ajipanga kufika mbali, kusaidia wengine


Na Victor Mkumbo

MIAKA inavyozidi kwenda ndivyo wimbi la wasanii linavyozidi kuwa kubwa, na hakuna ubishi juu ya hilo kwani miaka ya 1990 walikuwepo wasanii lakini wengi walikuwa kwenye makundi.


Ongezeko la wasanii haimaanishi kwamba vijana wengi wanakimbilia tasnia ya muziki au nyingine kwa sababu ya umaskini, ingawa kuna asilimia kadhaa ya vijana ambao hufanya kazi hiyo kwa sababu ya ugumu wa maisha.

Mwaka 1998 kijana anayetambulika kwa jina la Mathew Selestine a.k.a 'Mathew TBS Original', aliamua kuanza kufanya muziki, lakini miaka hiyo hakuwa akijihusha sana kwenye fani hiyo kwani alijikita zaidi kwenye uandishi wa filamu ambao kwa namna moja ama nyingine uliweza kumtangaza na kujulikana na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo.

Baada ya kuona kipaji chake cha uandishi wa filamu kinafanya vizuri, aliamua kukaa kimya kwa sababu ambazo zinaweza kuwa nje ya ya uwezo wake lakini bado wadau waliendelea kumsubua ili afanye muziki pia.

Katika kipindi hicho  alikuwa katika harakati za kutafuta maisha, lakini mwaka 2012 akaja rasmi kwenye tasnia ya muziki, ambapo sasa kibao chake cha 'Mchawi Hana Sababu', kimeanza kusikika na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio nchini.


Kutoka kwa kazi hiyo kuna mfanya msanii huyo kurudisha hisia za wadau ambao walikuwa wakimfahamu kijana huyo kama mwandishi wa filamu na kukumbuka aliwahi kutamka atakuja kufanya muziki na ndio ilikuwa ndoto yake kubwa.

Anasema kuwa awali kabisa miaka ya nyuma wakati akiwa kama mwandishi wa filamu aliweka wazi kuwa anapenda kufanya muziki, ingawa mama yake mzazi alikuwa ni mchezaji wa mpira netiboli kwa kipindi hicho.

Anasema kuwa sasa ameamua kuigia kwenye muziki ili kuwaonesha wadau wa tasnia hiyo namna muziki unavyotakiwa kufanywa kwani wasanii wengi waliopo sasa nyimbo za mapenzi ndizo wanazotoa ingawa kuna mambo mbalimbali ambayo watanzania wanatakiwa kupewa elimu na kutatua matatizo yao.

Sababu nyingine iliyomfanya ajikite katika muziki huo ni kuhitaji kuwaelimisha watanzania ambao bado hawajaelimika juu ya misingi bora ya maisha, ikiwemo Ujinga, Umaskini na Maradhi ambavyo vinawasumbua wengi.

"Najua baadhi ya wasanii wanajitahidi kufanya kazi zenye ujumbe zaidi lakini kwa upande wangu nakuja kama mkombozi wa maskini na kufungua njia za mafanikio si kwa kuwapa hela bali ujumbe ambao upatikana kwenye kazi zangu ndiyo jibu kwao," anasema Mathew.

Amasema kuwa kuwa pamoja  na kufika kimataifa kwanza kabisa anahitaji kuhakikisha kwamba watanzania wote wanamkubali ndipo safari ya kuelekea nje zitakapoanza.

Hata hivyo anasisitiza kuwa katika muziki wake atawakomboa na vijana wengine ambao wanapenda kufanya muziki, ili nao watimize malengo yao.

"Malego ni mengi lakini kikubwa natahitaji kwanza watanzania wanitambue na baada ya hapo nitakuwa katika harakati za kuvuka mipaka, kwa sababu huwezi kusema unataka kufika juu wakati hata chini hujui utapamaliza vipi," anasema.

Anaongeza kuwa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa hilo ndilo wazo lake na atahakikisha anakutana na wasanii ambao tayari wanajulikana, ili waweze kumpa mawazo na ushauri namna ya kufanya ili aweze kutimiza zaidi malengo yake.

Anasema kuwa alipofikia amekutana na changamoto mbalimbali lakini uvumilivu wake na kujituma ndio vimemfanya adumu mpaka leo.

Anasema kuwa katika maisha yake ya sanaa anaamini changomoto ni njia ya kumfanya aweze kufanya vizuri zaidi kwani wanaompa wakati mgumu ndiyo watu wanampa sababu ya yeye kubuni mbinu zaidi za kuweka kukubandilika na si kujulikana kwa njia za wizi wa sanaa.

Anasema kuwa kila kitu kina ugumu endapo unakuwa haujajipanga lakini kwa upande wake yupo tayari kwa kila kitu kwani ushindi huja baada ya kazi nzito.

"Ugumu wa soko upo lakini naamini kama unafanya kazi nzuri si dhani kama soko kwako litakuwa gumu napenda kusema kwamba muziki wa hip hop si wa kuimba mapenzi na najua kujipanga ili kwenda sawa na soko," anasema.

Anasema kuwa tabia ya mtu huwa haibandiliki na kutumia dawa za kulevya inatengemea na maisha ya msanii, lakini wapo wengine ambao wanakuja kutumia dawa hizo baada ya kuona mtu fulani anatumia, ingawa kwa upande wake hawazi kama anaweza kugusa dawa hizo, ambapo hupoteza maisha ya vijana wengi duniani kote.

Hata hivyo kwa upande wake alitoa ushauri kwa wasanii wengine kuwa kitendo cha kutumia dawa za kulevya kinaweza kuhatarisha maisha yao, kwani matumizi hayo yanapigwa vita na Serikali kila siku.

Msanii huyo tofauti na masuala ya muziki pia ni mwandishi mkubwa wa filamu na mfanya biashara.

Alisema kuwa alikatisha masomo yake baada ya kuumwa gafla ugonjwa wa kufa ganzi mifupa na macho kutokuona vizuri, ambapo alikaa miaka mitatu kitandani, huku baadhi ya jamaa zake walikata tamaa na kuhisi hatopona tena.

"Niliugua ghafla na kukaa miaka mitatu ndani bila kuona jua, hivyo baadhi ya watu walikata tamaa na kujua kuwa nitakufa wakati wowote lakini uwezo wa Mungu ndio uliniokoa na kuniamsha tena kitandani ambapo kwa sasa nipo katika hali nzuri" anasema.


No comments:

Post a Comment