28 December 2012

Mapenzi yaua askari Polisi







Na Eliasa Ally, Iringa

ASKARI wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa mwenye namba G 3679, PC Manase Samwel (23), ambaye kituo chake cha kazi kipo mkoani Dodoma, ameuawa baada ya kupigwa mateke na marungu hadi kufa.


Inadaiwa askari huyo ambaye alikuwa likizo, alizuiwa na dada
yake kuondoka na mwanamke aliyekuwa akinywa naye pombe
za kienyeji lakini alikataa ndipo walipokuja walinzi wa Misitu
ya Sao Hill, uliopo Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa na
kuanza kumshambulia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda, alisema tukio hilo limetokea Desemba
25 mwaka huu, kwenye kilabu cha pombe za kienyeji cha Lusasi, kilichopo, eneo la Sao Hill, Tarafa ya Ifwagi, wilayani humo.

Alisema askari huyo alipigwa na kuuawa saa mbili usiku kwenye Kijiji cha Mapogolo, akiwa na mwanamke ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.

“Mwanamke huyu alinyweshwa pombe za kienyeji na marehemu kwa makubaliano kuwa siku ya Krismasi wangekuwa wote, dada
wa huyu askari (bila kumtaja jina), hakupendezwa na kitendo
cha kaka yake kuondoka na mwanamke huyo,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, dada wa marehemu baada ya kuona kuna mvutano mkubwa, aliwaita mgambo wa kijiji hicho ili waende kumsaidia asiondoke na huyo mwanamke.

“Mgambo walipofika na kuona purukushani hizo, hawakuuliza chanzo bali walianza kumpiga marehemu kwa mateke, marungu
hadi alipozidiwa na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi ambako baada ya muda mfupi alifariki dunia kutokana na kutokwa damu nyingi kichwani kwa kipigo,” alisema.

Kamanda Kamuhanda aliwataja watu waliokamatwa kutokana na mauaji hayo kuwa ni Leonard Samwel (52), Isaack Sagala (36), Eleuteri Sengala (41), Wilbart Ngailo (31), Greyson Sagala (27)
na Dickson Makombe (30).

Alisema wote ni walinzi wa Misitu ya Sao Hill pamoja na mwanamke aliyekuwa na marehemu wakinywa pombe ambapo
mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mufindi.

“Watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote wakikabiliwa na shtaka la mauaji,” alisema.

4 comments:

  1. TUKIO HILO LIWE FUNDISHO KWA ASKARI WENGINE WENYE TABIA KAMA HIYO YA KUPENDA KUNYWA POMBE ZA KIENYEJI (MATAPUTAPU) NA KISHA KUOPOA WANAWAKE WANYWA MATAPUTAPU.WAKUMBUKE DHAMANA WALIYOPEWA NA JAMUHULI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA JAMII.KWA KUTAMBUA HILO NDIO MAANA SERIKALI IKAWAPA NAFUU KWA WANYWAJI KWA KUWAPA POMBE ZA KISASA KWA BEI NAFUU WENYEWE WANAITA BEI YA MOTISHA.WASIDHARIRISHE DHAMANA WALIYOPEWA KWA KUPENDA NAFUU ZAIDI.

    ReplyDelete
  2. ASKARI NI SAWA NA MTANZANIA YE YOTE WALA HANA TOFAUTI YO YOTE POMBE YOYOTE INALEWESHA NA HATA KAMA NI MATAPUTAPU MSHAHARA WA MAASKARI TUNAUJUA ILA LAMSINGI KUMWAGA DAMU YA MWENZIO SI MAADILI MEMA WALA SIO YA KUENDEKEZA NI YALE YALE YA SOMALIA BINADAMU KUCHINJWA KAMA KUKU SIO UBINADAMU

    ReplyDelete
  3. Hebu sheria ifuate mkondo wake si dada yake Marehemu wala hao wanao jiita maafwande wa MSITU.

    ReplyDelete