24 December 2012

Baba aliyebaka mtoto amakatwa



Na Steven William, Muheza

MTUHUMIWA anayedaiwa kumbaka mtoto wake wa kufikia, mwenye umri wa miaka mitatu, Bw. Yakob Raimond, mkazi wa Muheza, mkoani Tanga, amekamatwa na wananchi waliokuwa wakimsaka na kumkabidhi kwa Jeshi la Polisi, wilayani humo.


Wananchi hao walimkuta Bw. Raimond shambani katika Kijiji
cha Ngugwini ambako alikwenda kujificha baada ya kubaka
mtoto huyo na kumuharibu vibaya sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Costantine Massawe, alisema mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho katika Kijiji cha Paramba, Kitongoji cha Kwajumbe, Kata ya Kicheba na kukimbia.

Alisema wakazi wa kitongoji hicho walikuwa wakimsaka mtuhumiwa kwa nguvu zote baada ya kufanya tukio la aibu
na kufanikiwa kumkamata akiwa shambani amejificha.

Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho, wamelaani kitendo alichokifanya mtuhumiwa na kuomba sheria ichukuwe mkondo wake iwe fundicho kwa wengine wenye tabia hiyo.

Hata hivyo, mtoto huyo kwa sasa amelazwa katika Tospitali ya Wilaya akiendelea kupatiwa matibabu ambapo hali yake inaelezwa ni mbaya.

No comments:

Post a Comment