28 December 2012
Auawa kwa kupigwa shoka kichwani
Na Eliasa All, Iringa
WAKAZI wa Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, wamekubwa na hofu kubwa juu ya usalama wa maisha yao baada ya mkulima mmoja wilayani humo, Clement Mkuvasa (45), kuuawa kwa kupigwa shoka kichwani akidaiwa kujihusisha na uchawi.
Tukio hilo linadaiwa kutokea jana ambapo watu wasiofahamika, walimcharaka marehemu wakidai ni mchawi na mshirikiana
anayeua watu katika Kijiji cha Mapogolo, wilayani humo.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wananchi waliokuwa eneo la tukio, walisema Mkuvasa aliuawa Desemba 26 mwaka huu baada ya watu hao kumvizia mchaka wakati akirudi nyumbani kwake.
Walisema mauaji hayo yanawapa hofu kubwa kuhusu usalama wao na kudai kama marehemu alikuwa akijihusisha na mambo hayo angefikishwa katika vyombo husika badala ya kumuua kinyama.
Mkazi wa kijiji hicho, Bw. Leonald Mwakandale, alisema umefika wakati wa Serikali kuchukua hatua dhidi ya watu wanaohusika na mauaji ya aina hiyo na kudai marehemu alikuwa mtu mzuri katika jamii ya wakazi wa kijiji hicho.
Akizungmzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda, alisema marehemu alikatwa na shoka kichwani mara nne na watu wasiojulikana baada ya kumvamia.
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta watu hao ili waweze kufikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KUENDEKEZA UCHAWI NI DALILI WAKAZI WENGI HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA NI VEMA SERIKALI IELEZE KWENYE SENSA NI MIKOA IPI INA WATU WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA ILI KISOMO CHENYE MANUFAA KIANZE MARA MOJA WATU WA AINA HII WAO UTAPIAMLO,DEGEDEGE,KIFAFA,UKIMWI NA KULOGWA SI RAHISI KUPIGA HATUA YA MAENDELEO
ReplyDelete