22 November 2012

Wawili wafariki dunia DarLeah Daudi na Angelina Faustine

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti Jijini Dar es salaam, likiwemo la mtoto Praygod Emanueli(1) kudumbukia kwenye shimo la maji na kufariki papo hapo.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Bw.Charles kenyela alisema tukio hilo limetokea juzi maeneo ya mbezi beach ambapo mtoto huyo alipoteza maisha yake baada ya kudumbukia kwenye shimo la maji.
 
Kamanda Kenyela alisema ,shimo hilo lilichimbwa na jirani yao aliyefahamika kwa jina moja la shabani kwa ajili ya matumizi ya choo, hata hivyo halikufunikwa na kuachwa wazi kwa ajili ya kutoa maji machafu.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala,hakuna aliyekamatwa,upelelezi unaendelea.

Wakati huo huo huko maeneo ya Mbezi kwa Yusuph Kinondoni Gari namba T 823 ALH  Scania ikiendeshwa na Bw. Shabani Senzige(35)ikitokea Kibamba kuelekea Mbezi Mwisho, iliigonga pikipiki nanba T 265 BBE San LG, na kumsababishia kifo dereva wa pikipiki hiyo aliyetambulika kwa jina moja la Bw. Kinambo anayekadiriwa kuwa na umri kati (25-30).

Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela  alisema  mwili  wa marehenu umehifadhiwa hospitali ya Tumbi Kibaha dereva amekamatwa na upelelezi unaendeleaNo comments:

Post a Comment