22 November 2012

NDC kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe



Na Agnes Mwaijega

SHIRIKA la Maendeleo la Taifa (NDC) limesema limejipanga kuhakikisha linazalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe ili kupunguzu tatizo la nishati hiyo nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa NDC Bw.Alley Mwakibolwa alisema tayari wameshafanya utafiti wa kutosha ambao umeonesha kuwa makaa ya mawe yaliyoko Mchuchuma yataweza kuzalisha umeme wa megahati 600.

Alisema nchi imeshaanza kutumia makaa ya mawe yanapatikana nchini kutengeneza vitu mbalimbali na kuongeza kuwa gharama itakayotumika kwa ajili ya mradi huo ni dola bilioni 1.2 na tayari wameshaweka mikakati ya kuanza kuchimba makaa hayo.

"Sasa hivi hatutegemei makaa kutoka nje ya nchi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, ambapo makaa ya mawe tulikuwa tunayatoa Afrika ya Kusini tujipanga vizuri kuhakikisha kuwa makaa yetu yanatunufaisha," alisema.

Alisema uzalishaji wa umeme kwa sasa unatumia fedha nyingi na kusema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutapunguza gharama kubwa inayotumika kwa sasa.

Hata hivyo alisema katika kuhakikisha mradi huo unakuwa na mafanikio ni lazima miundo mbinu iboreshwe ili kurahisisha utendaji wa kazi.

No comments:

Post a Comment