26 November 2012

MSAJILI MAHAKAMA KANDA YA ZIWA AOMBA FAIRI KULICHUNGUZA


Na Timothy Itembe Tarime

MSAJILI wa Wilaya Mahakama kuu ya kanda ya ziwa Mwanza Tanzania ameitisha fairi
kesi No 57/2010 na No 7/2012 baina ya mdaiwa Mugore Mang'u na mdai Peter Zackaria
Kiyonge kuchunguza Shauri hilo ili kulitolea mwafaka.


Hali hiyo iliibuka punde tu baada ya mdaiwa Bw Mang'u kukamatiwa mali zake Gari yake
moja pamoja na mifugo (Ng'ombe) 21 na kuuzwa bila kushirikishwa hatimaye kuchukua
hatua za kwenda kulalamika katika ofisi ya  msajili mkuu wa kanda ya ziwa Mwanza
Tanzania ambapo aliomba kuitisha fairi za kesi hiyo ili kwenda kujua mwenendo mzima
wakesi.

Awali kesi hiyo iliendeshwa na Mahakama ya Mwanzo wilayani Tarime chini ya Hakimu
wake Samweli Gimeno ambapo mshitakiwa  Bw Mang'u alihukumiwa kulipa fidia kwa mdai
Bw Kiyonge Garama za biashara na uendeshaji kutokana na jinai No124/2009.

Kwa mjibu wa hukumu ya januari,31,2011 Mahakama pamoja na washauri wameridhika na
ushahidi uliotolewa na upande wa madai maana amefafanua jinsi madai yalivyo kwani
mdai amedhibitisha kuwa alikuwa mfanya biashara wa Duka LESENI NO B.01229704 ya
huko  Rorya Obwere hivyo Mahakama kwa pamoja imekubali kuwa mdai amedhibitisha dai
lake anapewa ushindi jinsi alivyo dai ambapo Mahakama ilimhukumu Bw Mang'u  kumlipa
fidia Bw Kiyonge  Tsh.milioni 7,475,000.

Kufuatia hukumu hiyo mdaiwa Bw Mang'u alikamatiwa Gari lake toyota colora PFD 587
15,02,2012,pamoja na Mifugo yake Ng'ombe 21 hapo Novembar,20,2012 yote ya Tsh
milioni 27.

Ambapo kufuatia hali hiyo Bw Mang'u Jana aliamua kutinga katika ofisi ya  Msajili wa
Wilaya Mahakama  kuu Kanda ya Ziwa Mwanza kulalamika  mali yake kuuzwa kwa kesi
ambayo alidai amebambikiwa ambayo haijui wala hakuhusika ambapo  Msajili huyo
ameitisha Fairi kufanyia uchunguzi.

Kwa upande wake Bw Mang'u alisema kuwa shauri hilo ni lakubambikiwa ambapo
aliongeza  kusema kuwa kuna mchezo umeibuka ambao wajanja wanaunda wa kuwanyang'anya
watu mali zao wanapo bumba vyesi kwa kumbambikia mtu mwenye mali ilimradi tu wapate
fedha ya kula hata kama hakuhusika.

''Ninashangaa kuona ni naingizwa katika kesi ambayo siijui wala sihusiki ambayo
nimeambiwa kuwa ninashitakiwa na kulipa garama za kesi sanjari na mali yake Bw
Kiyonge iliyo fungiwa ndani ya kibanda chini ya jinai kesi no124/2009 ambayo
ilifunguliwa Mahakama ya mwanzo Riagoro Wilayani Rorya Desembar,27,2101 ya kulipa
Fidia  Tsh milioni 7,45,000 kwa kosa ambalo silangu na wala sijawahi kuitwa
Mahakamani kuambiwa kuwa  ni natuhumiwa ili nikatoe  maelezo  ya kujitetea,ambapo
Mtu huyo ametumia jina langu kuwa ni nadaiwa kwa  shauri ambalo silielewi ambapo
hukumu hiyo ili pelekea kutaifishwa mali zangiu na kuuzwa mda mfupi bila
kushirikishwa''alisema Bw Mang'u.


No comments:

Post a Comment