22 November 2012

Afariki dunia kwa kujinyongaZubeda Mazunde na
Angelina Faustine.

MKAZI wa Ulongoni "B" Wilaya ya Ilala Dar es Saalam Mikidadi Shabani (37) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya manila.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda Mkoa wa Kipolisi Ilala, Bibi.Marietha Komba alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa saba usiku.

Alisema mtu huyo alikutwa nyumbani kwake akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya manila aliyokuwa ameitundika kwenye dari.

Kamanda Komba aliongeza kuwa eneo la tukio kulikutwa ngazi ambayo marehemu aliitumia kwa  kupanda juu ya dari pamoja na kamba za manila.

Kwa mujibu wa Kamanda Komba, marehemu aliacha ujumbe usemao " nimefanya hivi kwa maamuzi yangu mwenyewe" mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na upelezi bado unaendelea.

No comments:

Post a Comment