22 November 2012

Wanaosema CCM aijafanya chochote hawama jipya


Na Darlin Said

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mzimuni  Bw.Faraji Ngonyani amewashangaa wale wote wanaosema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakijafanya kazi yeyote na kusema kuwa hawana jipya.


Hayo aliyasema hivi karibuni katika hafla ya Kusimikwa Mlezi mpya wa Jumuiya wa wazazi CCM Bw.Othuman Kipeta katika kata hiyo.

Bw.Ngonyani aliyasema hayo alipokuwa akitoa ufafanuzi jinsi CCM ilivyojitahidi kuleta maendeleo katika Mtaa huo.

Alisema moja ya maendeleo yaliyoletwa na CCM ni kuwajengea Soko litakalogharimu Shilingi Milioni 600, ambapo halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni watawapatia pesa hizo kwa awamu tatu.

"Kwa kuanzia wameshatupatia Shilingi Mil.200 na  awamu mbili zilizobaki watatupatia baadaye"alisema. Bw.Ngonyani.

Alisema mkakati waliokuwa nao kwa sasa ni ifikapo mwaka 2013-2014 wanatafuta namna ya kuwawezesha watoto yatima,Wazee,Wajane na wale wote wanaofanana na makundi hayo.

Naye Diwani wa Kata ya Kawe, Bw.Othumani Kipeta alisema katika kuhakikisha wanatatua kero za wananchi Manispaa ya Kinondoni inatarajia ujenga daraja litakalowaunganisha wananchi wa Ukwamani na Mbezi Beach litakalogharimu Shilingi Milioni150.

Bw.Kipeta alisema mbali na ujenzi huo katika bajeti yake ya sasa wanatarajia kununua gari la wagonjwa  katika Zahanati ya Kawe baada ya kukamilisha ujenzi wa nyumba mbili za Madaktari katika Zahanati hiyo.

Sambamba na hilo Bw. Kipeta alisema Serikali imewapatia shilingi Milioni 17 kati ya hizo Milioni 7 zitatumika katika ujenzi wa ukuta uliopo katika eneo la Ukwamani na Milioni 10 zitatumika kuweka vifusi katika eneo la Mbezi Beach.No comments:

Post a Comment