24 September 2012
Taasisi za umma zatakiwa kutumia ramani mpya
Na Neema Malley
MKURUGENZI wa ramani na upimaji Ardhi Bw.Selassie Mayunga amezitaka taasisi za umma na zile za binafsi kutumia ramani mpya zilizotolewa na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya shughuli zao na kuachana na zile ramani zilizopo kwani zimeonyesha kupotosha ramani ya mipango miji.
Bw. Mayunga akiyasema hayo jana Dar es Salaam wakati wa mkutano wa watendaji wa upimaji wa ardhi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo aliwajulisha wananchi kuwa wizara imeandaa ramani mpya inayoonyesha mikoa yote 24
hivyo aliwaasa kuachana na ramani feki ambazo zinazambazwa na baadhi ya taasisi ambazo hazina mamlaka ya kazi hiyo.
"Nasema kuwa wenye mamlaka ya kutoa na kusambaza ramani ya miji ni Wizara ya ardhi peke yake hivyo wizara kwa kushirikiana na polisi hatutasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaye husika na usambazaji wa ramani hizo,"alisema.
Bw.Mayunga alisema onyo kwa kusema kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchapisha na kusambaza ramani bila kibali cha Wizara ya ardhi hivyo wao kama wizara watajitahidi kutafuta chanzo cha usambazaji wa ramani hizo.
Akizungumzia kuhusiana na tatizo la migogoro ya ardhi iliyokithili hapa nchini alisema kuwa linatoka na upimaji wa ardhi usiozingatia sheria ambao unafanywa kwa makusudi na wapima ramani kwa kutozingatia sheria ya ardhi.
Hivyo kwa kupitia mkutano huo Mkurugenzi huyo aliwataka wapima ardhi wote kupima ardhi kwa kufuata sheria za ardhi ili kupunguza migogoro hiyo au kutotokea kabisa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment