06 September 2012
Redd's Miss Ilala kupatikana kesho
Na Mwandishi Wetu
WASANII nguli wa kizazi kipya pamoja na Machozi Band, kesho watayapamba mashindano ya kumsaka 'Malkia wa Ilala' Redd's Miss Ilala 2012, yatakayofanyika kesho Nyumbani Lounge, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na mratibu wa mashindano hayo, Gadna G Habash ilieleza kuwa licha ya wasanii hao, MC katika kinyang'anyiro hicho atakuwa msanii anayeigiza sauti za viongozi mbalimbali maarufu, Steven Mengele 'Steve Nyerere'.
Habash alisema zawadi za washindi wa mashindano hayo, wanatarajia kutangaza leo.
Alisema mwaka huu Ilala inatarajia kutetea taji lake linaloshikiliwa na Salha Israel, ambaye ni Miss Tanzania 2011 kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya.
"Warembo wetu wote wako bomba na kila mmoja amejigamba kuvishwa taji hilo ambalo lipo Ilala, hivyo mashabiki wa urembo nchini wanatakiwa kufika kuona vipaji halisi," alisema.
Alisema wanyange hao wapo katika mazoezi kwa mwezi mmoja chini wakufunzi, Slyvia Mashuda ambaye ni Miss Tanzania namba mbili 2008 na Neema Mbuya pamoja na Dickson Daud wa THT katika shoo.
mashindano hayo yanadhaminiwa na Redd's Premmiun Cold, Uhuru One, Dodoma Wine, City Sports Lounge, Nyumbani Lounge, Times FM, Redio ya Cloud's FM na Amaya Salon.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment