25 September 2012
Mil. 100/- zatengwa kutoa elimu usalama kwa wanafunzi shuleni
Na Mariam Mziwanda
KAMPUNI ya mafuta ya Total, imetenga sh. milioni 10 ambazo zitatumika kutoa elimu ya usalama barabani katika shule mbalimbali nchini ili kupunguza vifo vya watoto vinavyotokana na ajali za barabarani.
Akizungumza kwenye mafunzo yaliyofanyika Dar es Salaam jana katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Meneja Sheria na Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Masha Msuya, alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuelewa sheria za usalama barabarani.
“Kampuni yetu imeona umuhimu wa kutoa mafunzo haya kutokana na changamoto nyingi zinazowapata watoto hasa wanaosoma shule zilizopo pembezoni mwa barabara,” alisema na kuongeza kuwa, shule 240 zilizopo Dar es salaam zitanufaika na mafunzo hayo.
Naye askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Kitengo cha Elimu, Habari na Uenezi aliyekuwa akitoa mafunzo hayo, Bw. Enock Machunde, amewataka watoto kufahamu umuhimu wa kuzingatia matumizi ya alama za barabarani.
Alisema jamii ikishirikiana na maderava wa magari, waanaweza kupunguza vifo vinavyotokana na ajali za barabarni kama kila mmoja atatimiza wajibu wake.
Mmoja wa wanafunzi hao, John James alisema wao ndio waathirika wakubwa wa ajali za barabani hivyo elimu hiyo ni muhimu kwao kujua mipaka na hatua za kuchukua wawapo barabarani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment