13 September 2012

Kalunde yatangaza mapambano



Na Mwandishi Wetu

BAADA ya kuitambulisha albamu yao mpya ya Imebaki stori, bendi ya Kalunde sasa imetangaza mapambano kuhakikisha ya kuzipa changamoto bendi nyingine za muziki wa dansi nchini.

Albamu hiyo mpya ina nyimbo za Imebaki stori iliyobeba jina la albamu, Fungua, Sisee, Ulinipendea nini, Njoo tucheze na Mama yangu.

Akizungumza Dar es Salaam jana kiongozi wa bendi hiyo, Bob Rudala alisema kutokana na ubora wa nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ana uhakika wataweza kushindana na bendi nyingine kongwe.

"Kiukweli kwa sasa tumeingia rasmi katika ushindani na tuna uhakika tutakuwa washindani wa kweli kutokana na 'vichwa' tulivyonavyo ndani ya Kalunde," alisema Rudala.

Rudala alisema hivi sasa wapo mbioni kuhakikisha wanaitambulisha albamu hiyo kila kumbi watakapokuwa wakitoa burudani wakianza keshokutwa katika Ukumbi wa Triniti, Osterbay.

Albamu hiyo ni ya pili kwa bendi hiyo, ya kwanza ni Hilda yenye nyimbo za Nitaka kuzaa na wewe, Itumbangwewe, Hilda iliyobeba jina la albamu na Fikiria. 


No comments:

Post a Comment