19 September 2012

CHANEDA yaandaa bonanza la utambulisho


Na Mwali Ibrahim

CHAMA cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA), kinaandaa bonanza maalumu kwa ajili kuutambulisha uongozi wake mpya ulioingia madarakani hivi karibuni.

Bonanza hilo linatarajia kufanyika Septemba 29 mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa CHANEDA, Michael Maurus alisema chama hicho kimepanga kuwatambulisha viongozi hao ili waweze wadau wa michezo wawatambue.

Alisema sambamba na utambulisho huo, pia bonanza hilo litazikutanisha timu za netiboli za Mkoa wa Dar es Salaam katika kunogesha tamasha hilo ambalo limelengo kukuza na kuendeleza mchezo huo.

"Uongozi huu umekuja upya na mikakati mipya, lakini yote ni kutaka kukuza zaidi na kuendeleza netiboli Dar es Salaam na nina imani kupitia bonanza hili timu zitachuana vyema na kuonesha upinzani wa kutosha," alisema.

Amezitaka timu kujitokeza kwa wingi katika bonanza hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Sadick.

No comments:

Post a Comment