21 August 2012

Zanztel yajumuika na watoto yatima



Na Mwandishi Wetu

WATOTO zaidi ya 100 kutoka kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hussein, jana walijumuika na wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, kusherehekea sikukuu ya Idi Pili iliyofanyika Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo iliyolenga kuwakutaanisha pamoja watoto hao na kuwapatia burudani mbalimbali kamae za muziki, kuruka kamba, kuimba, kukimbiza kuku na burudani nyinginezo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Deepak Gupta alisema kampuni yake inatambua hazina iliyopo kwa watoto na inahitaji kuendelezwa.

Alisema ili watoto waishio katika mazingira magumu wajitambue kuwa wanajaliwa, inatakiwa kuoneshwa upendo na kusikilizwa na kwa kulitambua hilo Zantel, imeamua kuwaandalia watoto hao hafla hiyo ili kuwafanya waione thamani yao katika jamii.

'Tumeandaa sherehe hii, ili kuwaonesha watoto na jamii nzima kwa ujumla kuwa watoto ni sehemu ya jamii, hivyo wanahitaji kuburudika kama watu wengine katika jamii," alisema Gupta.

Akizungumza katika sherehe hiyo, mlezi wa kituo cha Al-Hussein, Alhaji Mohammed Ghalibu alisema anawashukuru Zantel kwa kuwafanyia sherehe hiyo, ambayo hawajawahi kufanyiwa na kampuni yoyote.

"Watu wengi huwa wanatoa zawadi kabla ya sikukuu, lakini ni mara chache kampuni na watu binafsi huwa tayari kujumuika nasi siku kama hii," alisema Alhaji Ghalibu.

Zantel imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii, hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma bora na nafuu za mawasiliano.


No comments:

Post a Comment