02 August 2012

TEFA yaziita timu kuchukua fomu ligi ya TFF



Andrew Ignas na David John.

CHAMA cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke(TEFA),Kimezitaka timu zinazotarajia kushiriki Ligi ya TFF Ngazi ya wilaya kujitokeza kuchukua fomu za ushiriki.

Ligi ya TFF Ngazi ya wilaya kwa Temeke inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia  Septemba 7, mwaka huu katika viwanja mbalimbali vya Wilaya hiyo.


Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili jana Makamu Mwenyekiti wa TEFA Salehe Ndonga, alisema timu shiriki zinatakiwa kujitokeza kuchukua fomu za ushiriki wa ligi hiyo ambazo zilianza kutolewa kuanzia jana.

"Ligi yetu ya TFF kwa mwaka huu itaanza Septemba 7,ambapo fomu zitaanza kutolewa kuanzia leo (jana) mpaka Agosti 15, na mwisho wa kuridisha fomu ni mwishoni mwa mwezi huu,na usaili utafanyika Septemba 6,"alisema Ndonga.

Alisema  mashindano yanatarajiwa kutimua vumbi katika viwanja vitano ambavyo ni Twalipo Camp Wailes,Gonga(Kongowe),Yombo(kilakala),Abas Klabu (kurasini),na Mizinga(Kigamboni).

Wakati huo huo amelaani vikali tabia zinazofanywa na baadhi ya wachezaji kusajili zaidi ya timu moja.

"Kubwa lingine ambalo tutalifanyia kazi kuna baadhi ya wachezaji wanasajiliwa katika timu zaidi ya moja na wilaya tofauti tofauti hivyo tutawafungia wote watakaohusika na kashfa hiyo,"alisema

No comments:

Post a Comment