28 August 2012

Sera za kibenki zinazotungwa zitekelezwe kwa vitendo



Na Cornel Antony

UMASKINI uliokithiri na hali ngumu ya maisha nchini umesababisha wananchi wengi kuwa waoga na kukosa ubunifu ili kujikwamua na hali hiyo.

Pia, wengine huogopa kukopa fedha katika taasisi za fedha ili kuanzisha miradi kwa kukosa ufahamu wa mikopo.


Taasisi za fedha, zinatakiwa kuweka wazi sera na mipango yao kwa wananchi ili kuondoa hali hiyo ikiwemo ulipaji wa mikopo wanayochukua.

Wananchi wakipatiwa elimu ya ulipaji fedha hizo watajikwamua katika hali ngumu waliyonayo sasa.

Kupatikana kwa mikopo na huduma nyingine zimeiwezesha CRDB kuwa miongoni mwa benki bora nchini kwani huwapa wateja elimu ya mikopo hiyo.

Imekuwa ikitimiza vigezo vya huduma bora zinazohitajika au anazozihitaji mteja ikiwemo uanzishwaji wa matawi sehemu nyingi.

Mahitaji yake yanazidi kukua kutokana na ongezeko la watu ambapo wengi wao husafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo kutokana na  huduma bora.

Ni kweli hayati Baba wa Taifa alilipa kipaumbele toka uanzishwaji wake kwani walikabidhiwa majukumu ya kuinua uchumi wa kipato cha mwananchi wa vijijini na mjini yaani mwananchi wa kipato cha chini na mwananchi mwenye kipato kikubwa.


Kutokana na uwazi wake imekuwa ikifanya vizuri nchini bila kuyumba au kuteremka kiutendaji na kukua siku hadi siku huku ikibuni mbinu mbalimbali mpya zinazoendana na kasi ya maendeleo.

Katika Wilaya ya Mtwara, imesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa wakulima wa zao la korosho ambao hutoa fedha za kuwapatia vyama vya ushirika kununulia korosho.

Vyama vya ushirika (AMCOS) vimekuwa vikinunua na kukopa matrekta kwa masharti nafuu yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi, kutokana na usimamizi bora.

Miaka miwili sasa benki hiyo imeanzisha huduma nyingine ambayo imelenga zaidi kumkomboa mwanamke wa kitanzania kupitia akaunti ya malkia inayolenga maeneo mbalimbali ya kiuchumi.

Meneja wa tawi jipya la CRDB Masasi Bw.Erick Muchuruza    anasema kuwa akaunti ya malkia kweli ni mkombozi wa wajasiriamali wadogo na hata wakubwa kwani wateja hujiwekea kiwango chenye uwezo wake na baadae humpa fursa ya kukopa kirahisi zaidi.

"Mpaka sasa hivi tawi langu  nimepata wateja wengi wakifungua malkia akaunti, lakini nina changamoto kubwa ya kutoa elimu zaidi ili kuongeza idadi ya wateja kwa tawi hili jipya kwani halijafunguliwa rasmi, anasema Bw. Muchuruza  


"Lakini nimepata faraja kubwa ya kuona wateja kwa wingi kufungua akaunti zao tangu tarehe mwezi mei, mpaka sasa kwani nina akaunti zisizopungua 821 ambapo ni kipindi kifupi mno kupata," anasema.

  
Anasema, ni kweli usiopingika kuwa CRDB ni mkombozi wa wanyonge kwani walio wengi wametokea vijijini kufuata huduma Masasi pamoja na kukabiliwa na ushindani wa bank nyingine.

"Tunapata wateja wa kutoka wilaya ya Newala, Nanyumbu kwa mkoa wa Mtwara, Nachingwea na Rwangwa kutoka mkoa wa Lindi na Tunduru kutoka Mkoa wa Ruvuma,".
                 
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi. Farida Mgomi, na mteja wa akaunti ya malkia anausifia uamuzi wa kufungua tawi hilo kuwa ni wa busara na utasaidia wanawake wengi kujikwamua kiuchumi.

"Benki ya CRDB imenirahisishia kazi kwenye maendeleo ya wilaya yangu kwenye vyama vya ushirika na wateja mmoja mmoja walikuwa wanatembea kilomita 424 ili kupata huduma hiyo, sasa wamerahisishiwa," anasema.

Anawataka wnawake katika wilaya yake na wilaya jirani kufungua kufungua akaunti ya malkia kataika benki hiyo ili kupunguza makali ya maisha kwani mafanikio yake yanaonekana kwa uwazi zaidi.

"Nitatumia muda wangu mwingi kwa kila kona ya wilaya yangu kuwashauri kufungua akaunti ya malkia kwa idadi kubwa," anasema.

"Namshukuru Bw. Nasib Kalamba kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wakazi wilaya ya Masasi na wamemuelewa kuhusu elimu ya kibenki waliyoitoa kwa wakazi wangu, naomba nafasi hii ya  itolewe kila wakati hususani kwenye tawi hili jipya kwani anaeleweka kirahisi kwa wateja," anasema Bi. Mgomi.


Anasema, kiongozi huyo anakipaji cha kuelimisha wateja na kumuelewa kirahisi zaidi hivyo ni hazina ya benki hiyo tofauti na mameneje wengine ambao huwa na kauli mbaya kwa wateja.

CRDB ni moja ya benki inayoweza kusoma nyakati na ndio maana wanasifika kwa huduma bora kama watanzania wengi wangeenda na wakati.

Pamoja nia nzuri ya serikali kubinafsha mashirika hayo, yapo ayaliyofanya vizuri ambayo matunda yake yanaonekana hadi leo hii,ingawa mengi yaliishia kusiko julikana.

Benki ya CRDB ni miongoni mwa taasisi zilizo kuwa mali ya Serikali, kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa wazalenzo ili waweze kuiendesha kama sekta  binafsi kwa ajili ya kuiletea maendeleo jamii ya kitanzania.

Benki hiyo ilianzishwa mwaka 1947, ikiwa kama Benki ya Ardhi Tanganyika yaani Land Bank Of Tanganyika (LBT)ikiwa na mtaji wa milioni 4 kabla ya mwaka 1961 kuanzishwa Shirika la Mikopo ya Kilimo,Aglicuture Credit Agency(ACA)kwa ajili ya kuchukua nafasi ya LBT kwa lengo la kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo.

Hata hivyo mwaka 1964 serikali iliamua kubadili mfumo wa uendeshaji wa ACA  na kuanzishika Shirika la Taifa la Maendeleo ya Mikopo (NDCA), kwa ajili ya kuchukua nafasi ya ACA kabla ya mwaka 1971 , kuanzishwa kwa  Benki ya Tanzania ya Maendeleo vijijini.

Katika kipindi chote hicho benki hiyo ilikuwa chini ya usimamizi wa serikali huku ikiwa na mtaji wa shilingi milioni 25 za kitanzania.

Mwaka 1984 ndipo ilipoanzishwa Benki ya CRDB huku serikali ikiwa na  hisa asilimia 51 wakati asilimia 30 zilikuwa zinamilikiwa na vyama vya ushirika na asilimia 19 ikimilikiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Jina la benki ya CRDB lilitokana na uamuzi wa serikali wa mwaka 1996 wa kubinafsisha mashirika yake na kuwa ni ya watu binafsi.

Jina hilo pia Julai mwaka 1997 lilibadilishwa na kuwa CRDB Bank Ltd kwa ajili ya kulenga masoko yote ya ndani na nje ya nchi kabla ya kubadilishwa tena kuwa CRDB Bank PLC baada ya  mwaka 2009 hisa zake kuanza kuuzwa katika Tanganyika soko la hisa la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment