23 August 2012
NMB kudhamini 'Maisha Plus'
Na Darlin Said
BENKI ya NMB inatarajia kudhamini mashindano yatakayoendeshwa na Maisha Plus, kwa kushirikiana na Oxfam pamoja na washindi walioshinda katika kampeni ya Mama shujaa wa chakula iliyoendeshwa na Oxfam .
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mark Wiessing alisema NMB imeamua kudhamini mashindano hayo ili kuhakikisha ardhi iliyopo inamsaidia Mtanzania mwenyewe, kwani kupitia shindano hilo litawahamasisha watu kujishughulisha katika mambo ya kilimo.
"Kwa kuhakikisha NMB inawajali wakulima wadogo wadogo, imeanzisha NMB foundation ambayo mbali na kutoa elimu pia inawahamasisha kujiwekea akiba na kukopa kupitia," alisema
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Masoud Kipanya alisema mashindano ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidogo na yaliyopita, kwani idadi ya washiriki itaongezeka kutoka 18 miaka ya nyuma mpaka kufikia 26 mpaka 30 mwaka huu.
Alisema washiriki watakaa siku 14 na wataanza na wanawake walioshinda katika kampeni ya Mama Shujaa wa chakula, ambao watakaa siku 11 na siku tatu zitakazobaki watawajumuisha na washiriki wengine.
"Tumeamua kushirikiana na Mama Shujaa wa chakula ili kumuenzi mwanamke ambaye ndiye mkulima mdogo, ambaye mzalishaji mkuu wa chakula na kuwafanya vijana waweze kujifunza na kufikiria umuhimu wa uzalishaji wa chakula,"alisema Bw Kipanya
Alisema usaili unatarajia kuanza Jumatatu ijayo kwa kupitia zile sehemu ambazo wametoka washindi wa Mama Shujaa wa chakula kwa kuonesha dokumentari itakayoonesha wakulima hao shughuli zao walizokuwa wananzifanya katika uzalishaji wa chakula.
Naye Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Bi Monica Gorman alisema lengo la kushirikiana na Maisha Plus, ni kuweza kuwafanya wananchi wawaone wanawake hao kivipi wameweza kulima na kujipatia chakula chao cha nyumbani na biashara.
"Wanawake hawa wamejitahidi sana kuondoa umasikini,njaa kwa kulima huku wakikabiliwa na changamoto mbalimbali,"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment