17 August 2012
Kufungiwa MwanaHalisi ni sahihi-Pinda
Na Magreth Kinabo, Maelezo Dodoma
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema mtu yoyote ambaye anaona hakutendewa haki kuhusu kufungiwa gazeti la MwanaHalisi, anaweza kufafuta utaratibu mwingine wa kwenda mahakamani.
Bw. Pinda aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni , Bw. Freeman Mbowe.
Katika swali lake, Bw. Mbowe alisema Julai 30 mwaka huu, Serikali ililifungia gazeti hilo kwa muda usiojulikana kwa kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
“Kama Serikali inatambua umuhimu wa mahakama, kwanini imelifungia gazeti la hili badala ya kulipeleka mahakamani na wahusika wapate nafasi ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa?” alisema Bw. Mbowe.
Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema ni kweli Serikali imechukua uamuzi huo kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi na mtu yoyote kwa msingi wa sheria hiyo ambaye ataona hajatendewa haki ni juu yake kutafuta utaratibu mwingine wa kwenda mahakamani,” alisema Bw. Pinda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SERA YA GAZETI HILI NI KU-DISCUSS PEOPLE BADALA YA ISSUES KUNA USEMI SMALL MINDS DISCUSS PEOPLE ,AVERAGE MINDS DISCUSS ISSUES WHILE GREAT MINDS ACTS VYOMBO VYA HABARI MAJUNGU NA UMBEA SI MTAJI
ReplyDelete